Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » BI.SAMIA SULUHU HASSAN - MWANAMKE WA KWANZA KUSHIKA WADHFA WA MAKAMU RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Unapozungumzia Ushindi wa John Pombe Magufuli wa CCM anazungumzia pia fursa kwa Bi Samia Suluhu Hassani kuhudumia taifa hili la Afrika Mashariki kama mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa rais wa Tanzania.
 
Lakini Bi Samia ni nani na unaweza kumfahamu vipi?
  Tangu kongamano la Chama tawala nchini Tanzania CCM kumteua Daktari John Pombe Magufuli Joseph kuwa mshika bendera wa CCM, Chama hicho kiliweka historia kwa kumteua Bi Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza.
  Tangu Dodoma, Bi Samia aliwekwa kwenye ramani ya wanasiasa wanawake waliobobea barani Afrika.
  Bi Samia Suluhu ana umri wa miaka 54.
  Kwa wale wanaomjua Bi Samia wanasema kuwa ni mchache wa maneno. Asili yake ni Kisiwani Zanzibar.
  Bi Samia Suluhu Hassan amewahi kushikilia nyadhifa za uwaziri katika serikali ya Muungano wa Tanzania na kadhalika amewahi kutumikia serikali ya visiwani Zanzibar kama waziri katika afisi ya makamu wa rais.
  Ni mwanamke wa Kwanza kuwa Mgombea Mwenza na kushinda
Tangazo la kumtaja kama mgombea mwenza wa rais mteule wa tano wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania sasa limezaa matunda na kumuweka Bi Samia katika mstari wa mbele barani Afrika kama naibu rais wa Jamhuri ya Tanzania.
  Chama CCM pia kimeingia katika daftari la vyama vilivyowapa wanawake sauti katika serikali yake katika karne hii ya 21.
  Bi Samia alikamilisha masomo ya shule ya upili mwaka wa 1976 .
  Masomo
  Aliajiriwa kama mchapishaji katika wizara ya mipango na maendeleo ya nchi, kazi ambayo aliifanya huku akiendelea na masomo yake hadi alipohitimu katika chuo kikuu cha Manchester, Uingereza.
  Bi Samia anasema kuwa njia yake ya ufanisi haijakuwa rahisi kama inavyodhaniwa. ''Safari yangu katika siasa imekuwa njia ndefu na yenye tija.''
  Kimsingi ufanisi wangu katika siasa za Tanzania umetokana na uweledi na umakini katika kila jambo ninalolifanya.''
  ''Sio rahisi kuwajibikia familia yako wakati huohuo ukiendelea na maisha ya siasa elimu na majukumu mengine ya kikazi," anasema Bi Samia.
  Familia Aliolewa mwaka wa 1978, na Bw Hafidh Ameir, ambaye wakati huo alikuwa afisa wa Kilimo .
  Walijaliwa watoto wanne.
  Mmoja kati ya wanawe Wanu Hafidh Ameir (1982), ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar
  Siasa
  Bi samia alijiunga na siasa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2000.
  Wakati huo alijiunga na bunge la wawakilishi la Zanzibar kama mjumbe maalum. Haikuchukua muda nyota yake ikaanza kung'aa na akateuliwa kuwa waziri na rais Amani Karume.
  Alitumikia taifa hadi mwaka wa 2005 alipochaguliwa tena na kuteuliwa upya kama waziri.
  Mwaka wa 2010 alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi.
  Punde tu akateuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa waziri wa maswala ya muungano.
  Wadhifa aliohudumu hadi RAIS MTEULE Dkt John Pombe Magufuli alipomtangaza kuwa mgombea mwenza.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / BI.SAMIA SULUHU HASSAN - MWANAMKE WA KWANZA KUSHIKA WADHFA WA MAKAMU RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

No comments :