Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » KWA MUHTASARI PITIA HIZI HAPA UTAJIFUNZA KITU
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

zaidi ya watu mia tatu wakaazi wa kijiji cha kikombo mkoani dodoma wamebakia katika hali ya sinto fahamu baada ya mtu mmoja asiyejulikana kujimilikisha maeneo ya wanakijiji hao bila ya uongozi wa kijiji hicho kuwa na taarifa.

Wakizungumza na rasi fm wakaazi wa kijiji hicho wamesema kuwa mtu aitwaye Ernest Kato amejimilikisha maeneo pasipo kuwashirikisha wanakijiji hao nakutaka kuanza shughuli za uchimbaji wa mchanga jambo lililowafanya wanachi kuiomba wizara ya madini kuweza kuifuta leseni hiyo ili kuweza kuokoa vyanzo vya maji na mazingira.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

Kiwanda cha Saruji Tanga (Simba Cement), kimeingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania (TRL), kusafirisha shehena ya saruji kwa njia ya reli kutoka mkoani Tanga kwenda mikoa ya Mwanza na Kigoma.

Chini ya Makubaliano hayo zaidi ya tani laki nne na nusu zitasafirishwa kwa mwaka na hivyo kupunguza gharama ya bei ya Saruji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Magharibi kutokana na usafirishaji wa reli kuwa wa bei nafuu.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Ofisa mdhamini wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Ali Mohammed Dadi amesema mshindi wa uwakilishi katika Jimbo la Ziwani ni Suleiman Ali wa CCM na si Asaa Hamad wa UPDP aliyetangazwa awali.
Dadi kutoka ofisi ndogo ya Pemba amesema kuwa msimamizi wa uchaguzi katika Wilaya ya Chakechake, Othman Hamisi alikosea wakati wa kujaza karatasi ya matokeo ya mshindi wa jimbo hilo.

Ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) umeridhishwa na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Rais John Magufuli katika kuongeza juhudi za kupambana na rushwa. 

Hali hiyo itabadili mtazamo wa awali kwamba utawala bora ulishapotea nchini, kama ilivyoonekana katika tafiti nyingi zilizofanyika.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

Baada ya kumpata Meya wa Jiji la Dar es Salaam, mchakato wa kumchagua naibu meya umeanza.
Juzi, Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), Isaya Mwita alichaguliwa kuwa umeya akimshinda mpinzani wake Yusuph Yenga (CCM) kwa kura 84 dhidi ya 67.

Akizungumza jana, Meya Mwita alisema tarehe rasmi ya uchaguzi wa kumpata naibu meya haijafahamika na kwamba leo atashauriana na uongozi wa jiji na kwamba mara tu baada ya Sikukuu ya Pasaka ataitisha kikao cha baraza.
KIMATAIFA
Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter amesema shambulio lililofanyika dhidi ya Ubeligiji linabainisha wazi kwamba nchi za Ulaya zinatakiwa kuongeza kasi ya kutokomeza ugaidi.
Amesema kuwa makundi ya wapiganaji wa Kiislam nchini Syria na Iraq moja ya tishio kwa nchi ya Ulaya na kwamba yakiachwa yaendelee kustawi yatazitesa nchi za Ulaya

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa jana liliitisha kikao kujadili hali ya mambo nchini Burundi.

Kikao hicho kilichofanyika mjini Geneva Uswisi kilijadili ripoti ya wataalamu watatu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusiana na hali ya haki za binadamu nchini Burundi.

Asasi zisizo za kiserikali pamoja na nchi wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Burundi ianzishe mwenendo wa mazungumzo na wapinzani kwa shabaha ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.

NA
Kundi la wanamgambo wa Al Shabab limepiga marufuku uuzaji na ununuzi wa bidhaa zilizoundwa Uturuki nchini Somalia.
Al-Shabab imewaarifu wafanyibiashara katika majimbo ya Kusini mwa Somalia na maeneo ya Lower Shabelle kuwa bidhaa zinazotokea Uturuku ni haramu.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / KWA MUHTASARI PITIA HIZI HAPA UTAJIFUNZA KITU

No comments :