Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » SERIKALI YALIFUNGIA GAZETI LA MSETO KWA MIEZI 36, MATUSI NA UCHOCHEZI VYALIPONZA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kulifungia gazeti la Mseto kwa miezi 36 leo Agosti 11,2016 katika ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari MAELEZO  Bw.Vicent Tiganya.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kulifungia gazeti la Mseto kwa miezi 36 leo Agosti 11,2016 katika ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam huku waandishi wa habari wa kmsikiliza.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amelifungia gazeti la Mseto   kwa miezi 36 kutokana na kuchapisha habari za uongo na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali.
Uamuzi huo wa kulifungia gazeti la Mseto  umetolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 242 lilitolewa tarehe 10Agosti 2016 kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 Sura ya 229,Kifungu 25(1).
Mhe. Nape Moses Nnauye ameeleza kuwa Kifungu hicho kinampa mamlaka yeye kama Waziri kuchukua uamuzi wa kufungia Gazeti kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo wa kuandika na kuchapisha habari za uongo na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali.
“Serikali kwa masikitiko makubwa imelazimika kilifungia gazeti la Mseto  kutokana na mwenendo wa uandishi wa kuandika na kuchapisha habari za uongo na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali kwa nia ya kumchafua Rais  wetu wa Awamu ya Tano  Mhe.Dkt.John Pombe Mgufuli na viongozi wa Serikali” Alisema Mhe Waziri Nape.
Aidha Mhe. Nape amesema kuwa hatua ya kulifungia gazeti la Mseto imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda  mrefu kuanzia Septemba,2012 hadi Agosti,2016 kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kuacha kuandika  habari za upotoshaji,uchochezi na za uongo na zisizo zingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa Habari bila mafanikio.
Ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania imeridhia mikataba mbalimbali ya Kimataifa inayoanisha Uhuru wa Habari na mipaka ya habari kama vile tamko la Haki za Binaadamu la mwaka 1948 ambapo nchi yetu imeruhusu kwa kiwango kikubwa  kwa kuweka ukomo wa uhuru huo kwa kukataza habari za uzushi uongo na uchochezi.
Gazeti la Mseto limezuiwa kuchapishwa katika njia nyingine yeyote ikiwemo mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya  Kieletroniki na Posta Sura ya 306.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / SERIKALI YALIFUNGIA GAZETI LA MSETO KWA MIEZI 36, MATUSI NA UCHOCHEZI VYALIPONZA

No comments :