Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » WAKAZI WA CHAMWINO DODOMA WATAKA KUWEKWA KWA ALAMA ZA BARABARANI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na Peter Mkwavila,CHAMWINO.

WAKAZI wa kijiji cha Buigiri wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma wameiomba serikali kuweke vivuko vya kuvukia waenda kwa miguu na mifugo vya alama za barabarani ikiwemo na mabango ili kuepusha ajali za mara kwa mara zinazotokea katika eneo hilo.

Wakizungumza na Mtandao huu kwa nyakati tofauti wakazi hao ambao kijiji chao kipo kwenye barabara ya kutoka Dodoma kuelekea Morogoro,wameitaka serikali kwa kupitia wakala wake Tanroad kuwawekea alama hizo za vivuko vya barabarani ili waweze kuondokana na ajali zinazosababisha na madereva wa magari wanaoendesha kwa mwendo wa kasi .

Chigulu Masigati (65) ambaye ni mmoja wa wakazi wa kijiji hicho cha Buigiri liyeondokewa na mjukuu wake aliyemtaja kwa jila la Challo Kalima aliyegongwa na moja la basi lililokuwa safarini toka Shinyenga hadi Dar es salaam mapema wiki hii majira ya jioni.

Alisema kuwa kifo cha mjukuu wake huyo ni zaidi ya vifo 15 toka vitokee katika eneo hilo na vilivyotokea karibu vingi vimesababisha na mwendo kasi wa madereva wa mabasi hayo wanapokuwa barabarani.

Alisema pamoja na hatua ya serikali ya kuweka askari wa kikosi cha barabarani bado madereva hao wamekuwa hawajali kama kuna watu ambao wanaotakiwa kuangaliwa usalama wao katika kuepusha ajali hizo.

Magreth Matonya (55) alisema kuwa katika eneo hilo madereva wamekuwa wakikimbiza magari yao kutokana na kutokuwepo kwa alama za tahadhari na hata kama zipo zitakuwa zimefutika na hivyo zinatakiwa kuonekana.
“Ni muhimu kwa serikali kupitia wakala wake wa barabarani Tanroad kuhakikisha alama hizo zinaonekana ili madereva waweze kuheshimu alama hizo za vivuko ikiwemo hata na mabango ya yanayoonyesha eneo la kuvugia mifuko”alisema.

Alisema kuwa katika eneo la kijiji chao wamekuwa wakizika watu karibu walio wengi wanaosababisha kwa kukanyangwa na magari hii ni kutokana na wanaondesha kupita kwa mwendo usiozingatia hatari yoyote ule unayoweza kusababisha kutokea ajali.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo ya Buigiri Keneth Yindi alikiri na kusema kuwa kati ya viongozi ambao wanakerwa wananchi wake kugongwa mara kwa mara na magari ni yeye pamoja na kuwa ameshatoa taarifa kwa vyombo husika.

Alisema katika eneo hilo hakuna alama yoyote inayoonyesha kama kuna eneo la kuvukia watu na mifugo na kama ipo ni wakati sasa kwa mamlaka husika kuweka alama hizo ambazo ni muhimu kwa matumizi wa watu na mifugo.

“Kwa upande wangu tayari nimeshatoa taarifa kwa wahusika,lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa na badala yake watu wangu wanagongwa na magari hayo kutokana na mwendo kasi wanaopitanao kwenye eneo hilo pamoja na kuwa kikosi cha polisi wa barabarani kuwepo”alisema.

Mwisho

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / WAKAZI WA CHAMWINO DODOMA WATAKA KUWEKWA KWA ALAMA ZA BARABARANI

No comments :