Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » ‘PEDESHEE’ NDAMA KULA MWAKA MPYA LUPANGO
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Ndama Shaaban Hussein ‘Pedeshee Ndama’ (mwenye pingu) alipofikishwa mahakamani Kisutu leo.
DAR ES SALAAM: KESI  ya mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam,  Ndama Shaaban Hussein almaarufu “Pedeshee Ndama Mutoto ya Ng’ombe”, aliyewahi kuwa mfadhili wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia (Wazee wa Ngwasuma) leo imeahirishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Januari 6, 2017 kutokana na upelelezi wa polisi kutokamilika.
Ndama anatuhumiwa kutenda makosa sita ukiwemo  utapeli wa Dola za Marekani 540, 390 ambazo ni sawa na zaidi ya Shilingi bilioni moja za Tanzania.
Awali kesi yake ilipopanda mahakamani  hapo alisomewa mashtaka sita mbele ya Hakimu Victoria Nongwa na Mwendesha Mashtaka, Leonard Msigwa, akisaidiana na Christopher Challo kuwa mnamo Februari 20, 2014 mkoani Dar es Salaam,  Ndama alitengeneza nyaraka feki zikionyesha kupata kibali cha kusafirisha sampuli za madini ya dhahabu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).  Mashitaka ya pili, tatu na nne pia yalikuwa ya kugushi nyaraka, ikiwemo iliyotoka Umoja wa Mataifa  iliyodai kuisafisha kampuni yake ya Muru Platinum Tanzania Investment Company Ltd kuwa imeruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu.

Nyaraka hizo zililenga kuiaminisha Kampuni ya Trade TJL DTYL Ltd ya Australia kuwa Muru ni watu halali kwa biashara hiyo.
Anadaiwa pia ugushi nyaraka zilizoonyesha kuwa alilipa kiasi cha Dola 331, 200 sawa na Shilingi milioni 728 kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kama kodi ya kupitisha mzigo huo hapa nchini.

Shitaka la tano ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Dola 540,390 kutoka kampuni hiyo ya Australia zilizowekwa katika akaunti ya Kampuni ya Muru katika Benki ya Stanbic,  na shtaka la sita lilihusu utakatishaji wa fedha hizo.
Ndama alikana mashtaka yote akarudishwa rumande.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / ‘PEDESHEE’ NDAMA KULA MWAKA MPYA LUPANGO

No comments :