Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » EU WAITAKA KUWAHIFADHI WAHAMIAJI ZAIDI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker akiwa na Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan

Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya leo watakutana katika mkutano wa kilele, kujaribu kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa wahamiaji barani Ulaya pamoja na kuishawishi Uturuki kuwapa hifadhi wahamiaji wanaotokea Syria 

Mkutano huo wa kilele unalenga kufanya kazi pamoja na nchi zilizo nje ya mipaka ya bara la Ulaya ili bara hilo liweze kupambana na mgogoro mkubwa wa wahamiaji kuwahi kutokea tangu vita vya pili vya dunia.
Jambo muhimu litakalozingatiwa katika mkutano huo wa leo ni kuishawishi Uturuki kuukubali mpango wa Umoja wa ulaya, unaoitaka nchi hiyo kuwapa hifadhi wahamiaji milioni mbili, huku Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa anelekea nchini humo Jumapili kwa ajili ya mazungumzo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa katika bunge la Ujerumani - Bundestag
Kabla ya mkutano huo wa kilele, Merkel amesema Uturuki ina jukumu muhimu katika kuutatua mgogoro wa wahamiaji, na kwamba nchi za Ulaya zinahitajika kuisaidia zaidi nchi hiyo kupambana na ongezeko hilo la wahamiaji.

Merkel ameongeza kwamba lazima kuwepo mshikamano barani Ulaya juu ya mgogoro wa wahamiaji
Wakati huo huo, Makamu wa Rais wa Umoja wa Ulaya Frans Timmermans pamoja na maafisa waandamizi wingineo, wamewasili Uturuki jana kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kukubali mpango huo wa Umoja wa Ulaya, baada ya kuahirisha safari hiyo kutokana na shambulio la mabomu la mjini Ankara mwishoni mwa juma lilopita.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / EU WAITAKA KUWAHIFADHI WAHAMIAJI ZAIDI

No comments :