Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » ICC NA KENYA DHIDI YA RAIA WAKE
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Kenya inaendeleza harakati kali za kidiplomasia kujaribu kuzishawishi nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuizuia korti hiyo ya kimataifa kuendelea na kesi dhidi ya raia wake wawili akiwemo Naibu Rais, William Ruto.

Nchi zilizosaini mkataba wa Roma uliopelekea kuanzishwa ICC zinatarajiwa kukutana wiki hii kutathmini utendaji wa mahakama hiyo. Kenya imekuwa ikizishawishi nchi za Afrika kuunga mkono mabadiliko ya sheria na kanuni za uendeshwaji wa korti hiyo ili kuathiri mwenendo wa kesi zinazomkabili Naibu Rais wa nchi hiyo William Ruto na mwanahabari Joshua arap Sang.

Viongozi wakuu wa ICC akiwemo mwendesha mashtaka, Fatou Bensouda wametoa wito kwa nchi wanachama kutochukua hatua zozote zitakazohujumu uhuru wa korti hiyo. Kwenye taarifa yao, viongozi wa ICC wamesema kuhujumu uhuru wa mahakama hiyo kutapelekea kushitadi mwenendo wa kupuuzwa sheria za kimataifa.

Naibu Rais wa Kenya, William Ruto na mwanahabari, Joshua Sang wanakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu 1400 walipoteza maisha.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / ICC NA KENYA DHIDI YA RAIA WAKE

No comments :