Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » HIZI HAPA KIMATAIFA USIKU WA DECEMBER 07/2015
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

ufaransa

Uchaguzi huo umefanyika wakati nchi hiyo ikiwa katika sheria ya hali ya dharura iliyowekwa wiki tatu zilizipita baada ya kufanyika mashambulizi ya wenye itikadi kali yaliyosababisha watu 130 kuuwawa mjini Paris.

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia FN kinachoongozwa na Marine Le Pen ambaye kitaaluma ni mwanasheria kimejipatia ushindi huo mkubwa kabisa wa kiasi asilimia 28 kote Ufaransa na kuibuka kidedea katika orodha ya vyama vilivyoingia kwenye uchaguzi huo katika majimbo alau sita kati ya 13 kwa mujibu wa makadirio ya mwisho ya matokeo yaliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani.

Ushindi huo umevunja rekodi ya asilimia 40 iliyowekwa na chama hicho huko nyuma katika majimbo hayo,matokeo ambayo yametokana zaidi na hasira za wapiga kura kuhusiana na suala la kudumaa kwa uchumi na khofu ya usalama inayohusishwa na mgogoro wa wimbi la wakimbizi barani Ulaya.Marine Le Pen ameyapokea matokeo hayo kwa furaha kubwa na kusema ni matokeo makubwa akisema yamedhihirisha chama chake cha FN ni nambari moja na hakina mpinzani nchini Ufaransa.
"Watu wa Ufaransa wamejieleza .Na kwa mujibu watu wa nchi hii,Ufaransa inanyanyua kichwa.Matokeo ya uchaguzi huu yanathibitisha kile ambacho kilionekana katika chaguzi zilizopita lakini waangalizi rasmi bado hawakutaka kukitambua . FN hakina mpinzani na ndio chama cha Ufaransa,wakati ambapo hakina uwakilishi imara bungeni''

dwswahili.com 

***************************************************************************************
 
syria

Serikali ya Syria imesema shambulio ambalo limedaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa muungano unaoongozwa na Marekani, na ambalo lilisababisha vifo vya wanajeshi watatu wa Syria, ni uchokozi.

Damascus imelitaka Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati kuzuia kujirudia kwa kisa kama hicho.

Muungano unaoongozwa na Marekani umekanusha kushambulia kambi ya jeshi mkoa wa Deir al-Zor mashariki mwa Syria.

Majeshi ya serikali yanadhibiti sehemu ya mkoa huo, sehemu nyingine zikidhibitiwa na wapiganaji wanaojiita Islamic State.

Viongozi wa wamekuwa wakihimiza majeshi yanayoshambulia wapiganaji Syria kushirikiana na kuratibu mashambulio kwa pamoja.

bbcswahili.com 

**************************************************************************************************
 
ufaransa

Mazungumzo ya kimataifa yanayoongozwa na Umoja wa mataifa juu ya kumnusuru binaadamu na athari za ongezeko la joto duniani, leo yanaingia katika hatua muhimu. 

Mawaziri kutoka takriban nchi 195 zinazoshiriki katika mkutano huo unaolenga kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi, wanaanza wiki ya mazungumzo kabambe ya kujaribu kufikia makubaliano ya kihistoria mjini Paris, Ufaransa. 

Makubaliano hayo muhimu yanalenga kuanzisha kutumika kwa nishati ambayo haitoi gesi chafu badala ya nishati inayotumika sasa ya kutoka kwa makaa, mafuta na gesi. 

Akizungmza hapo jana katika makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatikan, Papa Francis amesema anaomba viongozi wawe na ujasiri wa kufikia maamuzi magumu lakini muhimu zaidi kuwaokoa wanadamu. 

Mazungumzo hayo ya Paris yalianza mnamo tarehe 30 mwezi Novemba na yanatarajiwa kukamilika Ijumaa ijayo.

dwswahili 

************************************************************************************************

kenya

Wakaazi wa mji wa Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya wanasema wamegundua zaidi ya miili 20 iliyozikwa kwenye makaburi ya jumla.

Miongoni mwa miili hiyo ni ule wa mama mmoja aliyeripotiwa kupotea siku tano zilizopita.
Picha za kusikitisha zilisambaa mitandaonii asubuhi ya leo, zikionyesha sehemu za mwili za watu zikichomoza kutoka makaburi yaliyochimbwa juu juu.

Miili mingine ilikuwa uchi. Mwili wa mama ulioonekana kuharibiwa ulizua hisia nzito zaidi.
Marehemu asemekana alikuwa mama wawatoto watano, aliyekamatwa na watu wasiojulikana siku nne zilizopita.

Seneta wa eneo hilo Billow Kerrow alieleza ugunduzi huo kama wa kutisha, na kudai waliouwawa ni waathirika wa mauaji ya serikali.

Inspekta mkuu polisi Joseph Boinnet alidhibitisha kifo cha mwanamke huyo, lakini akakanusha madai kuwa kuna makaburi ya jumla.

Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yanaamini kuwa askari wa kupambana na ugaidi kwa kawaida kuwaua washukiwa.

Aidha wamekashifu vyombo vya usalama kwa kupuuza taratibu za kisheria na kuwaua mashahidi kabla ya kesi zao kumalizika.

Serikali imewahi kuitaja mahakama kama bodi inayovunja guu vita dhidi ya ugaidi.

Mwaka jana Makamu wa Rais William Ruto alisema washukiwa wa ugaidi huachiliwa kwa dhamana kwa urahisi sana wanapofikishwa mahakamani , kisha wao hutoweka wasionekane tena.

Mnamo Mwezi mwei, miili kumi na moja ilipatikana kwenye makaburi mjini wajiri, kusini mwa Mandera.

Mabaki ya risasi yaliyopatikana kando ya makaburi hayo yalizua shauku zaidi kuwa huenda polisi wa kupambana na ugaidi walihusika.

bbcswahili 

******************************************************************************************************

Uganda

Huduma ya gari moshi ya kubeba abiria imerejea mjini Kampala Uganda kwa mara ya kwanza tangu 1998
Gari moshi hilo lenye mabehewa 5 litakuwa linahudumu kutoka katikati ya mji mkuu wa Kampala na kwenda takriban kilomita 14 nje ya mji huo.

Watu wachache waliojua kuhusu kurejea kwa huduma hiyo walifika katika kituo cha gari moshi cha Kampala.

Safari hiyo inapitia katika vitongoji vya mji huo ambao kwa sasa haipitiki kwa sababu ya mijengo mingi.
Japo huduma hiyo ni mpya gari moshi lenyewe ni nzee mno na hata rangi mpya iliyopakwa kwenye mabehewa hayo matano yanayotumika haijakauuka vyema.

Safari ya mkondo mmoja inagharimu senti 45 kwa dola. 

Reli nchini Uganda ilijengwa miaka ya mwanzomwanzo ya 1900 na wakoloni kutoka Uingereza.
Wakati huo reli hiyo ilikuwa na dhumuni kuu ya kubeba mali ghafi kuipeleka katika bandari ya Mombasa nchini Kenya na kisha kusafirishwa kwa meli hadi Uingereza.

Muundo msingi wa reli hiyo haujaboreshwa kwa kiasi kikubwa mbali na kusafisha tu haswa baada ya mgogoro wa kisiasa uliopelekea kuvunjika kwa muungano wa Afrika Mashariki miaka ya 1970.

 bbcswahili
****************************************************************************************************
  
Marekani

Rais wa Marekani Barack Obama ameapa kuwa nchi yake italiangamiza kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Dola la Kiislamu IS na kuwasaka wafuasi wa kundi hilo nchini Marekani na kwengineko. 

Akilihutubia taifa la Marekani hapo jana, Obama amesema baada ya vita vingi, raia wengi wa Marekani wanajiuliza maswali iwapo wanakabiliwa na saratani ambayo haina tiba ya haraka akiongeza shambulizi la San Bernadino ambapo watu 14 waliuawa wiki iliyopita, ni thibitisho dhahiri kuwa kitisho cha ugaidi nchini Marekani kinaongezeka. 

Obama amesema kitisho cha ugaidi ni suala halisi lakini amewahakikishia raia wake kuwa atapambana vililivo na magaidi. 

Kiongozi huyo wa Marekani amewatolea wito Waislamu nchini Marekani na kote duniani kupinga kwa kauli moja itikadi kali zinazoenezwa na makundi kama IS na mtandao wa kigaidi wa Al  Qaeda.

dwswahili
***************************************************************************************************

Iraq

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amewasili mapema leo katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad katika ziara ya kushtukiza kutokana na sababu za kiusalama. 

Steinmeier anatarajiwa kuiahidi serikali ya Iraq kuwa Ujerumani itaisaidia kupambana dhidi ya wanamgambo wa Dola la Kiislamu IS. 

Alipowasili, Steinmeier amesema uthabiti wa Iraq ni muhimu kama kutafutwa kwa suluhisho la kisiasa Syria na kuongeza Ujerumani itasimama na nchi hiyo katika nyakati ngumu. 

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani atakutana na Rais wa Iraq Fuad Masum na Waziri Mkuu Haider al Abadi. 

Wanamgambo wa IS wanayadhibiti sehemu kubwa ya Iraq.

dwswahili
*********************************************************************************************************

Venezuela

Muungano wa vyama vya upinzani nchini Venezuela umeshinda uchaguzi wa bunge, huo ukiwa ushindi mkubwa zaidi kwa upinzani katika kipindi cha miaka 16 iliyopita. 

Wapiga kura wameiadhibu serikali ya kisosholisti inayoongozwa na Rais Nicolas Maduro katika uchaguzi huo wa bunge kwa kushindwa kushughulikia mgogoro wa kiuchumi na kudorora kwa usalama katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta. 

Rais Maduro amekubali kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi huo ambao ni pigo kubwa kwa utawala wake. 

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Venezuela Tibisay Lucena ametangaza Muungano wa vyama vya upinzani wa Democratic Unity Roundtable MUD umeshinda viti 99 kati ya viti jumla 167 vya bunge huku chama cha Maduro cha United Socialist Party of Venezuela kikipata viti 46. Wafuasi wa upinzani wamesherehekea ushindi huo katika mji mkuu Caracas. 

Rwanda

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema ataamua iwapo atagombea muhula wa tatu madarakani au la, baada ya kura ya maoni kufanyika nchini humo ya kuifanyia marekebisho Katiba ili kumruhusu kugombea urais kwa muhula mwingine. 

Katika mkutano na maafisa wakuu wa chama chake cha Rwanda Patriotic Front hapo jana, Kagame amesema maamuzi yake yatajikita katika matokeo ya kura ya maoni inayotarajiwa kuendeshwa mwezi huu. 

Iwapo kura hiyo ya maoni itafanikiwa, Rais Kagame ataruhusiwa kikatiba kugombea muhula wa tatu wa miaka saba katika uchaguzi mkuu mwaka 2017 na baadaye kugombea mihula mingine miwili ya miaka mitano kila mmoja ikimaanisha huenda akasalia madarakani hadi mwaka 2034. 

Marekani ambayo ni mojawapo ya wafadhili wakuu wa Rwanda imemtaka Kiongozi huyo kuonyesha mfano mwema katika kanda hiyo ya Afrika Mashariki kwa kuondoka madarakani akimaliza muhula wake wa sasa 2017.  

dwswahili
*******************************************************************************************************

Somalia
Raia wa Marekani ambaye alijiunga na kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab nchini Somalia amekamatwa.

Afisa wa serikali ya Somalia amesema kwamba Mwamerika huyo alikamatwa na wanajeshi kusini magharibi mwa Mogadishu akiwatoroka wapiganaji pinzani wa Kiislamu.

Hii ni baada ya wenzake kuuawa kwenye vita vya kambi pinzani ndani ya kundi hilo.

Mkuu wa wilaya ya Barawe Hussein Barre Mohamed amesema ingawa mwanamume huyo amekuwa Somalia wka muda mrefu, hakuweza kuzungumza Kisomali.

Kundi la Al-Shabab huegemea mtandao wa al-Qaeda, lakini baadhi ya makundi yamehama na kujiunga na kundi linalojiita Islamic State.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / HIZI HAPA KIMATAIFA USIKU WA DECEMBER 07/2015

No comments :