Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » CHOO KIMOJA WATUMIAJI ZAIDI YA 200, SHULE YA MKOANI DODOMA HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA...
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

picha haihusiana na habari
Elimu bure kwa sasa ndio wimbo upendwao na wengi wananchi wa kitanzania, lakini pia wasomi na wanaosema walichosikia wametoa changamoto lukuki juu ya elimu bure sasa moja kati ya changamoto hizo ipo katika shule ya sekondarI Nzuguni B Mjini dodoma.

Walimu na wanafunzi wa shule ya msingi  Nzuguni B wanaishi kwa kumwomba Mungu ili awanusuru na magonjwa ya mlipuko kutokana na tundu moja la choo kutumiwa na wanafunzi zaidi ya mia mbili huku walimu wa shule hiyo wakikosa vyoo.

Akizungumza kwa masikitika  mwalimu mkuu wa shule hiyo Liliani Luiva amesema wameamua kuishi kwa kumwomba Mungu kutokana na idadi hiyo ya wanafunzi kujisaidia kwenye tundu moja la choo huku wakikanyaga vinyesi  vya wenzao na kisha kwenda madarasani na viatu vilevile vilivyokanyaga vinyesi  na  kukaa chini kwa idadi hiyo hiyo ya wanafunzi.

Amesema  ongezeko la  idadi hiyo ya wanafunzi iliyotokana na mwitikio mkubwa wa wazazi  kuwaandikisha watoto wengi kutokana na mwito wa serikali wa elimu bure huku kukiwa hakuna ongezeko la miundombinu ye yote ikiwemo vyoo.

Aidha mwalimu huyo amesema mazingira ya shule hiyo sio rafiki kwa kufundishia   wanafunzi kutokana na shule hiyo kukosa uzio.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Joseph Masinga  amesema wanafunzi hao wanasoma katika mazingira hatarishi kutokana na mwingiliano wa watu unaotokana na eneo la shule hiyo kutopimwa hivyo kukosa hati miliki hali inayosababisha wenyeji kujenga mpaka karibu na maeneo ya shule hiyo.

Mwandishi: Lydia Kishia na John Banda
Mhariri: Denis J. Kazenzele
Tarehe: march 03.2016

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / CHOO KIMOJA WATUMIAJI ZAIDI YA 200, SHULE YA MKOANI DODOMA HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA...

No comments :