Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » BITUNI MSANGI: UTAMADUNI WA KUJISAIDIA VICHAKANI MWISHO
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma Bituni Msangi  amesema utamaduni wa wananchi kujisaidia vichakani umepungua na hivyo kupunguza idadi ya wanaougua magonjwa yanayotokana na uchafu.

Alitoa kauli hiyo juzi katika hotuba yake iliyosomwa  kwa niaba yake na Ofisa Tarafa Wilaya ya Kongwa Denis Semindu wakati wa kusherehekea mafanikio ya kufikia utimilifu wa Usafi wa mazingira katika kijiji Ugogoni yenye kauli mbiu Mazingira Safi yasiyokuwa na kinyesi.

Alisema kabla ya mradi wa Usafi wa Mazingira Tanzania (UMATA) kuanza wananchi wengi wa Wilaya hiyo walikuwa hawana vyoo na hivyo kujisaidia kwenye vyoo vya majirani au kwenye vichaka,porini, hivyo kufanya uchafuzi mkubwa katika vyanzo  vya maji na mazingira kwa ujumla.

"Hali hiyo ilichangia kwa kiasi kikubwa magonjwa ya kuharisha, kipindupindu  na yale yanayotokana na maji machafu" alisema.

alisema  kabla ya Mradi huu wa UMATA kijiji cha Ugogoni hakikuwa kwenye hali nzuri ya usafi wa mazingira licha ya kufanyiwa uhamasishaji wa mara kwa mara. 

Alisema kutokana na takwimu zilizokusanywa na kamati mnamo tarehe Oktoba 30, 2015 Kijiji kilikuwa na takribani kaya 229, ambapo kati ya kaya hizi ni kaya 11 tu hazikuwa na vyoo na kaya 61 tu ndizo zilikuwa na vifaa vya kunawia mikono (kibuyu chirizi). 

Pia alisema mpaka kufikia Desemba 20, 2015 kijiji kilikuwa na asilimia 100 ya kaya zote kuwa na kutumia vyoo, uwepo wa vifaa vya kunawia mikono baada ya kutoka chooni, mashimo ya taka na vibuyu chirizi

Akisoma risala ya Shirika la SAWA, Asnat Charles alisema  shirika hilo linahusika na uhamasishaji wa ujenzi na matumizi ya vyoo bora na kuchochea mabadiliko ya tabia za usafi katika jamii na shuleni kwa kutumia mbinu ya kushirikishi.

Pia Mradi umejikita kutoa elimu ya afya na usafi wa mazingira kwa shule za msingi ikimlenga mtotoambaye ndiye chachu ya mabadiliko kwa mtoto mwenzake, ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.  

Ofisa Afya Kata ya Ugogoni, Iqubal Janja alisema mila na desturi zilisababisha watu wengi wasiwe na vyoo na kujisaidia vichakani na magonjwa yaliyotokana na uchafu yalikuwa mengi.

Mwandishi: John Banda
Mhariri: Denis J. Kazenzele
Tarehe: march 03.2016

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / BITUNI MSANGI: UTAMADUNI WA KUJISAIDIA VICHAKANI MWISHO

No comments :