Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » HIZI HAPA NI ZA KIMATAIFA UNAWEZA KUZISOMA KABLA HUJALALA ....
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

Wakazi wa eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameomba kuzidishwa idadi ya wanajeshi katika eneo hilo ili kuwalinda. 

Wakazi wa eneo la Shabunda katika mkoa wa Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameiomba serikali ya nchi hiyo iongeze idadi ya wanajeshi katika eneo hilo. 

Drid Bambabwenge Msemaji wa wakazi wa eneo la Habunda ameeleza kusikitishwa na jinai zilizofanywa na wanajeshi kwa jina la "Raia Mutomboki" khususan katika barabara ya Burhale-Shabunda. 

Bambabwenge amewatuhumu wanamgambo wa "Raia Mutomboki" kwa kuwapora, kuwateka nyara na kufanya mashambulizi ya kuvizia dhidi ya raia. 

Hii ni katika hali ambayo eneo la mashariki mwa Kongo tangu miaka 20 iliyopita hadi sasa limeathiriwa na machafuko kufuatia kuwepo makundi ya waasi. 

Eneo hilo linaendelea kuathiriwa na machafuko kufuatia kushindwa jeshi la Kongo na wanajeshi wa kofia bluu wa Umoja wa Mataifa kuwaangamiza wanamgambo hao.

MAREKANI
 
Mgombea wa Democratic Hillary Clinton na mgombea wa Republican Donald Trump wameshinda majimbo mengi katika mchujo wa kuteua wagombea urais Marekani katika vyama vyao Jumanne Kuu.

Wagombea wote wawili wameshinda majimbo saba kila mmoja. Wameshinda wote wawili majimbo ya Alabama, Georgia, Tennessee na Virginia.

Bi Clinton pia ameshinda Arkansas na Texas, naye Bw Trump akashinda Massachusetts.

Bw Trump hata hivyo ameshindwa na Seneta Ted Cruz majimbo ya Texas, Alaska na Oklahoma.

Mgombea wa Democratic Bernie Sanders naye ameshinda kwake nyumbani katika jimbo la Vermont, Minnesota, Colorado na pia katika jimbo la Oklahoma.

Mchujo wa Jumanne Kuu hushuhudia majimbo 11 yakifanya mchujo kwa pamoja huku maandalizi ya uchaguzi mkuu tarehe 8 Novemba yakiendelea kushika kasi.

Bi Hillary Clinton, aliyekuwa wakati mmoja waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, pamoja na mfanyabiashara tajiri kutoka New York Donald Trump walipigiwa upatu kushinda majimbo mengi Jumanne Kuu.

Utafiti wa maoni ya baada ya kura ulikuwa umeonyesha Trump na gavana wa Ohio John Kasich wakikabiliana vikali katika mchujo wa chama cha Republican jimbo la Vermont, lakini baadaye Trump aliibuka mshindi.

Bi Clinton na Bw Sanders pia walikabiliana vikali katika jimbo la Massachusetts, kaskazini mashariki mwa Marekani lakini Clinton akaibuka mbabe.

 Bbcswahili.com

UGANDA
Forum for Democratic Change - FDC - ambacho mshika bendera wake Dr Kiiza Besigye bado anazuiliwa nyumbani kwake na vikosi vya usalama kimetoa masharti kadhaa ili kutuliza hali ya kisiasa ambayo inaendelea nchini Uganda tangu matokeo ya uchaguzi wa Febuari 18.

FDC kimetaka vikosi vya usalama kuacha kuzingira sio tu nyumba na mshika bendera wake lakini pia na ofisi zao.

Mkuu wa chama hicho, Meja Jerali Mustaafu Mugisha Muntu, mbele ya waandishi habari katika makao ya chama hicho mtaa wa Najanankubi mjini Kampala ametaka serikali itoe mzingiro katika nyumba ya Dkt Kizza Besigye.

FDC inadai kuwa wafuasi wake zaidi ya 300 baadhi wakiwa mawakala wamekuwa wakikamatwa kiholela nchini kote.

Aidha kinashuku matokeo ya uchaguzi ambayo yalitangazwa na tume ya uchaguzi iliompa ushindi Museveni, huku Meja Jenerali Mugisha akitoa sababu ya kuunda kwa tume hiyo.

Hata hivyo amepinga wazo la kutumia mabavu kufikia malengo yao akisema kuwa hiyo sio njia yao.

 Bbcswahili.com

ZIMBABWE
Gazeti la serikali - Herald - linaariifu kuwa waendesha mashtaka wamewarudishia mashtaka wanajeshi wawili wanaotuhumiwa kulilipuwa kwa bomu la petroli shamba la maziwa linalomilikiwa na familia ya rais Robert Mugabe.

Linaarifu kwamba, hatua hiyo inakiuka uamuzi wa mwendesha mashtaka mkuu kutupilia mbali mashtaka hayo dhidi ya wanajeshi hao wenye umri wa miaka ya 29 na 37.

Mawakili wa wanajeshi hao wanashinikiza kesi itupiliwe mbali wakieleza kuwa haiwezekani kwa Tomana kugeuza kauli yake na kuamuru washtakiwe.

Herald imeripoti, mawakili wa serikali wanasema naibu wa Tomana alichukua uamuzi huo wa kuwashtaki upya wanajeshi hao baada ya kufuata sheria zinazazohitajika.

Tomana ameachiliwa kwa dhaman baada ya uamuzii wake kumsababisha kushtakiwa kwa kuzuia sheria itendeke.

Amekana mashtaka.

Bbcswahili.com

TUMALIZIE NA HII YA KUHUSU NYWELE ZENYE MVI.

Wanasayansi wamebaini jeni inayosababisha nyewele kuwa na mvi,ugunduzi ambao unaweza kutoa njia mbadala za kuchelewesha ama hata kuzuia ishara hiyo ya uzee.

Upakaji rangi wa nywele unaweza kuzuia lakini utafiti huo wa jeni huenda ukazizuia nyewle kaa hizo kumea.

Kundi la kimataifa la wanasayansi lilichukua violezo vya DNA vya takriban watu 6000 waliojitolea kutoka Ulaya,Marekani na Waafrika.

Jeni hiyo aina ya IRF4 husimamia nywele za kawaida,ngozi na rangi ya macho inayoitwa Melanin.

Mwanasayansi kutoka katika chuo cha London alisema:tayari tunajua jeni kadhaa zinazozohusishwa na kumea kwa upara, na rangi ya nywele na jeni zinazosababisha umbile la nywele.

 Bbcswahili.com

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / HIZI HAPA NI ZA KIMATAIFA UNAWEZA KUZISOMA KABLA HUJALALA ....

No comments :