Na: geofrey stephen-Moshi.
Kesi ya wanasiasa maarufu nchini akiwemo Mwenyekiti wa TLP Dr Augustino Lyatonga Mrema na mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia wote wakiwa wameshakuwa wabunge wa jimbo la Vunjo kwa vipindi tofauti jana imeingia siku ya pili na kuvuta umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Moshi.
Siku ya juzi march 14.2016 ilikuwa siku maalumu kwa Jaji Mussa Mwandabo kutolea maamuzi ya hoja iliyoletwa na wakili wa mkuu wa serekali Mark Mwalambo mahakamani hapo kuhusiana na sheria inayowataka upande wa walalamikaji kupeleka kiapo cha mashahidi wa kesi hiyo ndani ya masaa 48 kwa mujibu wa sheria ya kesi ya uchaguzi iliyotungwa mwaka 2012 ambapo juzi kesi hiyo iliarishwa mpaka jana majira ya saa tatu na nusu asubuhi ilipoitwa tena.
Hata hivyo Jaji alitoa maamuzi ya kuwapa masaa 48 ambapo aliagiza upande wa mlalamikaji Dr Agustino Lyatonga Mrema chini ya wakili wake January Mkoboko kuakikisha mpaka siku ya ijumaa saa 10:30 asubuhi wanawakilisha viapo vya mashaidi wao 25 ikiwa imefungwa katika bahasha na kukabidhi mahakamani
Mlalamikaji katika kesi hiyo Dr Mrema alitolea ufafanuzi kuhusiana na hoja iliyowekwa na upande wa walalamikiwa kuwa Mrema amevunja katiba ya chama chake cha TLP na kusema kuwa aliamua kumuunga mkono mgombea wa CCm kwa sababu alitumia busara kuangalia kiongozi anayefaa kuwa Rais miongoni mwa wagombea nane waliokuwepo.
kesi hiyo itaanza kusikilizwa mfululizo siku ya jumatatu March 21 mwaka huu baada ya wakili wa serekali Mark Mwalambo kuomba kesi hiyo isikilizwe baada ya wiki ya pasaka na jaji kukataa na kutoa amri ya kesi kuanza haraka kusikilizwa siku ya jumatatu majira ya saa tatu kamili asubuhi .
MWISHO
No comments
Post a Comment