picha maktaba- sio halisi |
DODOMA
Jeshi la polisi
Mkoani Dodoma limefanikiwa kukamata silaha 26 aina ya Gobole na mitambo ya
kuyatengezea silaha hizo kinyume cha sheria ya umiliki wa siraha.
Kamanda wa polisi Mkoa
wa Dodoma Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari kuwa Magobore 19
yamesalimishwa na wamiliki waliokuwa wakiyamiliki kinyume na sheria baada ya
kusikia wito wa Jeshi hilo lililowataka kuzisalimisha.
Mambosasa amesema
jeshi hilo pia linawashikilia watu 7 wakazi wa Manda Wilayani Chamwino baada ya
kuwakamata na aina hiyo ya silaha 7 pamoja nyundo 1na risasi zilizotengenezwa
kienyeji ambazo zinadaiwa zilikuwa zikitumiwa kuwindia wanyama katika pori la
Ruaha mkoani iringa.
Aidha kamanda huyo
amesema moja ya Gobole lilikuwa limevishwa shanga ambayo ni ishara ya nguvu za
Giza ili polisi wasifanikiwe kuikamata ambapo pamoja na hilo wamefanikiwa
kukamata pikipiki zenye makosa mbalimba 250 na kuwatoza wamiliki wake jumla ya
million 7 na Laki 2 na 30 Elfu.
CHANZO: LYDIA KISHIA/JOHN BANDA
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Mbunge wa
jimbo la Bunda,Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza
na kulazimika kulala rumande baada ya kunyimwa dhamana.
Polisi wamevamia Hoteli aliyofikia
mbunge huyo na kumkamata majira ya saa 7 usiku na kisha kumpeleka
kituo cha kati cha Jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee, Joyce
Sokombe pamoja na Wakili John Malya.
Wabunge hao pamoja na uongozi wa juu wa Chadema Wako jijini Mwanza
Wabunge hao pamoja na uongozi wa juu wa Chadema Wako jijini Mwanza
kwa ajili ya kikao cha
Baraza Kuu la chama hicho kinachofanyika leo katika Hotel
ya Gold Crest.
Kikao hicho pia kinatarajiwa kumpata
katibu mkuu mpya kushika nafasi iliyoachwa wazi na Dokta Wilbroad Slaa
aliyejiuzuru mwaka uliopita baada ya kushindwa kuelewana katika baadhi ya
maamuzi na uongozi wa chama hicho.
CHANZO: MPEKUZIHURU
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
DAR ES SALAAM
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wa wizara yake kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani Serikali ya imejipanga kutumia sekta ya miundombinu kukuza na kufungua fursa za kiuchumi.
Akizungumza katika kikao kazi kilichohusisha Sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Mbarawa amemtaka kila mtu afanye kazi kwa umoja, uwazi na uadilifu ili kufikia lengo la kuanzishwa kwa wizara hiyo na kujihakikishia nafasi ya kuendelea kuwa mtumishi wa umma.
Amesema kila mfanyakazi atapewa malengo na atapimwa kulingana na malengo aliyopewa ili kuona iwapo utumishi wake unakidhi mahitaji ya Serikali kuwahudumia watanzania nchi inayojiandaa kuwa nchi ya kipato cha kati.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amewataka wafanyakazi kuwa na maono katika majukumu yao na kujitathimini kila wakati ili kubaini mafanikio na changamoto na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inaundwa na sekta tatu na inasimamia taasisi 29 zenye muelekeo wa ujenzi na usimamizi wa miundombinu na inatarajiwa kuiandaa Tanzania kuwa na miundombinu ya kisasa itakayowezesha kuhimili changamoto za kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
CHANZO: FULLSHANGWE
Makaratasi hayo yaliyochapishwa nchini Afrika Kusini yamewasili jana na kupokewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC huku tume hiyo ikitangaza kuwa maandalizi yote ya uchaguzi huo yamekamilika na kwamba, uchaguzi huo wa marudio utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.5.
Karatasi hizo zina picha za wagombea wote 14 wa kiti cha Urais wa Zanzibar licha ya baadhi ya wagombea akiwemo mgombea wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kwamba, hatogombea katika uchaguzi huo wa marudio.
Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliingia katika mgogoro wa kisiasa mwezi Oktoba mwaka jana baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi kwa kile alichokiita ukiukwaji wa sheria na taratibu wakati wa zoezi la upigaji kura.
Uchaguzi wa marudio Zanzibar unatarajiwa kufanyika march 20 huku vyama tisa kati ya 14 vilivyoshiriki katika uchaguzi uliofutwa wa Oktoba 25, kikiwemo chama cha CUF ambacho kinadai mgombea wake wa urais Maalim Seif Sharif Hamad ndiye mshindi halali wa kiti hicho vikiwa vimeshatangaza rasmi kwamba, havitashiriki katika uchaguzi huo.
No comments
Post a Comment