Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » UNAJUA SIRI Y AMWANAJESHI KUONGOZA MKOA WA KAGERA? SIRI HIYO NI HII HAPA!!!
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoboa siri ya kuteuliwa mwanajeshi kuongoza Mkoa wa Kagera, moja ya mikoa iliyoko pembezoni na yenye tishio kubwa la wahamiaji haramu na matatizo ya ardhi.

Hivi karibuni, Rais John Magufuli alifanya uteuzi wa wakuu wa mikoa 26 ya Tanzania Bara na kumteua Meja Jenerali mstaafu, Salum Mustafa Kijuu kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera.

Mbali ya Meja Jenerali mstaafu Kijuu, Rais Magufuli pia aliwateua wanajeshi wengine watatu kuongoza mikoa ya Katavi, Geita na Kigoma katika uteuzi huo wa Machi 13. 

Hao ni Meja Jenerali mstaafu, Ezekiel Kyunga (Geita), Meja Jenerali mstaafu, Raphael Muhuga (Katavi) na Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga (Kigoma).

Akifanya majumuisho ya ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera wiki iliyopita, Waziri Mkuu Majaliwa alisema: “Hapa kwenu Kagera kuna tatizo kubwa la waharamiaji haramu na uvamizi wa ardhi.

"Wavamizi wengine wanalima bangi katika maeneo yetu badala ya kufuga na kulima.

 “Waondoeni au punguzeni maeneo yao na lindeni mipaka yetu. Mapori ya Kimisi na Burigi yamegeuzwa maficho ya wahamiaji haramu,” alieleza Waziri Mkuu.

“Ndio maana tumemleta Meja Jenerali Kijuu. Shughuli yake huyu siyo nyepesi. Atatembea mwenyewe huko. Huyu si alikuwa Kamandi ya Infantry (askari wa miguu), kwa hiyo ataimudu shughuli hii vizuri.”

Mkoa huo umewahi pia kuongozwa na wakuu wa mikoa ambao ni wanajeshi katika miaka ya nyuma na baadhi yao ni Abdallah Twalipo, Tumainieli Kiwelu, Ayoub Simba, Fabian Massawe, Silas Mayunga na Enos Mfuru.

Mkoa wa Kagera unakabiliwa na tishio kubwa la wahamiaji haramu wanaingia nchini kutoka nchi jirani na wanamiliki ardhi kinyume cha sheria kutokana na udhaifu wa viongozi waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia.

Unapakana na Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Aidha, Waziri Mkuu aliiagiza Idara ya Uhamiaji nchini hasa mkoani Kagera kubadilika ambapo alihoji kwa nini hawavai sare za jeshi lao na kuingia msituni kusaka wahamiaji haramu badala yake wanavaa suti maofisini.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / UNAJUA SIRI Y AMWANAJESHI KUONGOZA MKOA WA KAGERA? SIRI HIYO NI HII HAPA!!!

No comments :