Jeshi
la Polisi mkoani Kagera limelazimika kutumia nguvu kuwatawanya wanafunzi
zaidi ya mia nane wa kidato cha tano na cha sita katika shule ya
sekondari ya Ihungo waliofanya maandamamo yasiyo rasmi wakati wakielekea
kwa mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Bukoba kwa lengo la kuelezea
matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo shuleni hapo yanayohusina na
masuala ya chakula, afya na taaluma.
Jeshi la Polisi lililazimika kutumia nguvu za kuwatawanya wanafunzi hao waliokuwa wakiiba nyimbo mbalimbali huku wapiga kelele baada ya kukaidi maekezo yaliyokuwa yanatolewa na maofisa wa jeshi hilo yaliyokuwa yanawataka watawanyike ili matatizo yao yatafutiwe ufumbuzi.
Awali, wakizungumza wakati wakielezea matatizo yaliyowapekelekea hadi wakafikia uamzi wa kuchukua hatua ya kuandamana kwa lengo la kuonana na mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Bukoba wanafunzi hao wameelezea kuwa wanapewa chakula kisichofaa kwa matumizi ya binadamu na wakati mwingine wanapewa mulo mmoja au milo miwili badala ya milo mitatu iliyopangwa pia wamelalamikia hali ya vyoo kwa kusema vinahatarisha afya zao kwa kuwa ni vibovu na hivyo vinaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa.
Naye, Philip Boneventula mkuu wa shule ya sekondari ya Ihungo akizungumza amesema malalamiko ya wanafunzi ni ya kweli, amesema tatizo la chakula linaloikabili shule hiyo linatokana na hatua ya wazabuni ya kusitisha huduma ya usambazaji wa chakula kufuatia deni kubwa wanalodai shule la zaidi ya shilingi milioni mia moja kumi na tatu, huku afisa taaluma wa sekondari katika manispaa ya Bukoba, Wandela Lwakatare kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Bukoba akielezea mambo yanayochangia matatizo yanayozikumba shule za sekondari za bweni za serikali ambayo ameyataja kuwa ni pamoja na ucheleweshwaji wa ruzuku.
Via>>ITV
No comments
Post a Comment