MEXICO
Miili ya watu wapatao 19 imepatikana katika jimbo la Mexico la Guerrero, ambako wanafunzi 43 walitoweka mwaka jana.
Polisi wanasema miili hiyo ilitupwa kwenye mto mwembamba, wenye kina cha mita mia tano katikati ya miamba na miti karibu na kijiji cha Chichi-hua-lco.
Miili nane kati ya hiyo ilikuwa inaonekana kuchomwa baadhi ya viungo.
Vipimo vya DNA vinatarajiwa kuchukuliwa kutoka katika familia za wanafunzi hao waliokufa, kuweza kujua kama ni kweli ni hao, ambao hawajapatikana mpaka sasa.&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
COLOMBIA
Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos amesema makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na waasi wa FARC ni hatua kubwa katika juhudi za kufanikisha kutiwa saini kwa mkataba wa amani mwezi Machi mwakani.
Akihutubia kwa njia ya televisheni, Rais Santos amesema pande hizo mbili zimeafikiana katika mambo manne kati ya matano.
Makubaliano haya ya sasa yanawaweka waathirika wa mzozo wa nchini humo katika hali ya matumaini ya kufikiwa kwa mchakato wa amani.
Watu takriban 200,000 wamepoteza maisha kutokana na mzozo na wengine milioni sita wanakadiriwa kuyakimbia makazi yao.&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
ZIMBABWE
Mbunge mmoja wa chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe amefikishwa kortini kujibu tuhuma za kumvunjia heshima mke wa Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo.
Mbunge Justice Wadyajena anadaiwa kumtusi Bi. Grace Mugabe wakati wa mkutano wa chama hicho katika mji wa Victoria Falls. "Ondoka hapa wewe mjinga kama huyo 'Mama' yako", Wadyajena anasemekana alimwambia mwanachama mwingine wa ZANU-PF aliyekuwa amevalia fulana yenye picha ya Bi. Grace.
Mke wa Rais wa Zimbabwe amepewa jina la 'Mama' ndani ya chama tawala na inasemekana kuwa ana ushawishi mkubwa mno ndani ya chama hicho na kwenye serikali kwa ujumla.
Ingawa wengi wameiona kesi hiyo kama ya kipuuzi, wachambuzi wa masuala ya sheria wanasema mbunge Justice Wadyajena anaweza kupoteza nafasi yake ya ubunge endapo atapatikana na hatia.
Rais Robert Mugabe ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1980 amekuwa akiwachukulia hatua kali wanasiasa wanoonekana kuingilia masuala ya familia yake.
Wadadisi wanasema mkwaruzano kati ya Grace Mugabe na makamu wa zamani wa Rais, Joyce Mujuru ndiyo iliyomfanya Rais Mugabe kumpiga kalamu Bi. Mujuru mwaka uliopita.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
GENEVA
Pande zinazo zozana Yemen zimeanza mazungumzo ya
kutafuta amani leo mjini Geneva, Uswisi katika juhudi za kuutafutia ufumbuzi
mzozo wa Yemen huku makubaliano ya kusitisha mapigano yakianza kutekelezwa.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Ahmad Fawzi amewaambia
wanahabari kuwa mazungumzo hayo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa yanalenga
kupatikana kwa suluhisho la kudumu kuhusu mzozo wa Yemen kwa kutoa mazingira
salama ya kibindamu, kusitisha mapigano na kurejea kwa utawala wa amani na
unaoeleweka kisiasa.
Juhudi za hapo awali za kuutatua mzozo huo ambao
umesababisha vifo vya zaidi ya watu 5,000 zilishindwa kuondoa tofauti za pande
zinazozana. Fawzi amesema washauri sita na wajumbe 12 wanashiriki katika
mazungumzo hayo.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
KENYA
Kenya ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa shirika la
kimataifa la biashara WTO imesema mawaziri wa biashara wanaokutana katika
mkutano huo wa siku nne ulioanza leo mjini Nairobi, wanapaswa kuamua iwapo
shirika la WTO liendelee kusimamia makubaliano makubwa ya kibiashara ambayo
yanaonekana kuwa magumu kufikiwa.
Shirika hilo lenye makao yake mjini Geneva na ambalo
lina zaidi ya nchi wanachama 160 limekuwa likijaribu kufikia makubaliano ya kibiashara
mapana na makhususi ya kuondoa vizuizi vya kibiashara tangu mkutano wa Doha
mwaka 2001 bila ya mafanikio makubwa.
Lengo la mkutano huo wa Nairobi ni kuamua ni jinsi
gani WTO itasonga mbele baada ya miaka kadhaa ya kutoweza kupiga hatua ya maana.
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed
amesema shirika hilo halijawa la tija kwa wanachamna wake hasa nchi zinazostawi
ambazo zitanufaika iwapo vikwazo vya kibiashara vitaondolewa ili kuweza kufikia
soko la kimataifa bila ya masharti magumu mno.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
UJERUMAN
Polisi wa Ujerumani wamemkamata mmoja wa wahubiri
mashuhuri wa kiislamu kwa madai ya kuliunga mkono kundi la kigadi linalopigana
nchini Syria.
Mhubiri huyo raia wa Ujerumani kwa jina Sven Lau
mwenye umri wa miaka 35 anashutumiwa kwa kuunga mkono vitendo vya kigaidi na
kuwasajili wapiganaji kwa ajili ya kundi lenye makao yake Syria la Jaish al
Muhajireen wal Ansar ambalo Ujerumani imeliorodhesha kama kundi la kigaidi.
Waendesha mashitaka wamesema mwaka 2013, Lau alikuwa
mwakilishi wa kundi hilo nchini Ujerumani na aliwasajili watu wawili kujiunga
na kundi hilo na pia anashitakiwa kwa kutuma euro 250 kwa mpiganaji raia wa
Ujerumani aliye Syria.
Lau amekamatwa katika jimbo la North Rhine
Westphalia.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
UTURUKI
Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema
uhusiano kati ya nchi yake na Umoja wa Ulaya umeimarika pakubwa tangu mkutano
wa kilele kati ya Uturuki na Umoja huo uliofanyika hivi karibuni.
Katika mkutano wa pamoja na Waziri mkuu wa Bulgaria
mjini Sofia, Davutoglu amewaambia wanahabari kuwa ukurasa mpya umefunguliwa
kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya baada ya kipindi cha miaka minne.
Umoja wa Ulaya hapo jana ulianza kushughulikia
mchakato wa nchi hiyo kujiunga na Umoja huo kama mwanachama ikiwa ni sehemu ya
makubaliano ya kusaidia kuukabili mzozo wa wahamiaji barani Ulaya.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
UCHINA
Barua iliyoandikwa na kiongozi wa chama cha Kikomunisti cha Uchina Mao Zedong akimwandikia kiongozi wa chama cha Leba cha Uingereza imeuzwa £605,000 ($918,000) kwenye mnada.
Kwenye barua hiyo ya mwaka 1937, Mao anamuomba Clement Attlee usaidizi katika kukabiliana na wanajeshi wa Japan waliokuwa wamevamia Uchina.
Wanadi wa bidhaa Sotheby wamesema barua hiyo ni ya thamani kubwa kutokana na saini ya Mao.
Bei ya mwisho ilizidi sana bei iliyotarajiwa ya £100,000-150,000.
Mnunuzi ni raia wa Uchina anayekusanya vitu vya kale.
Mao Zedong alizaliwa 1893 na ni mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Kikomunisti cha Uchina na mwanafalsafa msifika wa karne ya 20.Alisaidia kuunga jeshi la Uchina kwa jina Red Army, na kuwaongoza kutembelea maili 6,000 kutoroka maadui wao.
Baada ya ushindi 1949, Mao alitangaza kuundwa kwa Jamhuri ya Watu wa Uchina na akawa kiongozi wa kwanza. Sera zake zilisababisha vifo vya mamilioni ya watu.
No comments
Post a Comment