Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUJENGA OFISI ZA MAKAO MAKUU DODOMA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na Peter Mkwavila,Dodoma.

TUME ya Taifa ya uchaguzi jana ilikabidhiwa eneo la kiwanja na Mamlaka ya Ustawishaji Makao  Makuu  Dodoma (CDA) kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya makao makuu ambayo itakuwa mjini hapa.

Akizungumza jana mara baada ya kukagua eneo la ekari 10 ambalo litatumika kujenga ofisi hizo Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema  sasa tume inaenda kufikia lengo lake la kuwa na ofisi Mjini Dodoma.

Alisema ofisi yake pamoja na makamishna wa tume wamefika hapokwa ajili ya  kuliona eneo hilo la kiwanja na tumeridhika na tutakinunua kwa Sh. Milioni 470 kama tulivyoelezwa na CDA wenyewe.

Alisema lengo hilo lilikuwa la muda mrefukuwa na jengo la kutosheleza mahitaji kwani sasa ofisi ya tume hiyo iliyooo jijini Dar es Salaam ina ofisi tatu maeneo matatu tofauti lakini sasa wanatakiwa kufanya kazi eneo moja.

Alisema katika uchaguzi unaokuja watafanya shughuli za usimamizi wakiwa mjini Dodoma.

Naye Afisa Uwekezaji CDA, kwa upande wake Abeid Msangi alisema tume hiyo imepatiwa kiwanja cha ekari 10 ambacho kimezungukwa na barabara ya lami pande zote.

Alisema tume ya taifa ya uchagui wameleta maombi yao na mamlaka ya ustawishaji wa makao makuu imewapatia kiwanja eneo la uwekezaji la Inumbu lililopo Njedengwa na kwenye eneo hili lina miundombinu yote, maji umeme na barabara na sasa tunawaandalia hati.

Alisema jumla ya ekari 1500 zimetengwa katika eneo hilo na kuwekewa miundombinu mingine na kuzitaka ofisi za serikali kwenda CDA kutafuta maeneo kwa ajili ya kujenga ofisi zao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa uchaguzi wa tume hiyo, Kailima Ramadhani alisema katika uchaguzi mkuu uliopita walibakiza fedha kiasi cha bilioni 12 ambazo walimrudishia rais John Magufuli kwa ajili ya matumizi mewngine lakini lengo lilikuwa ni kujibana ili wawe na ofisi zao.

Alisema Rais Magufuli alitoa wazo la wao kuhamia Dodoma ili watekeleze maleng ya serikali kuhakia Dodoma.

Alisema eneo hilo lina miundombinu yote na wameanza mazungumzo la Wakala wa majengo (TBA) ili ifikapo Oktoba uenzi uanze na baada ya mwaka moja tuyme iwe na jengo lake

Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga alisema kama wakala na msimamizi mkuu wa majengo ya serikali watashirikiana na tume kuona azma yao inatimia.

Mwisho

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUJENGA OFISI ZA MAKAO MAKUU DODOMA

No comments :