TUME ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeaswa kuhakikisha tafiti zinazofanywa zijikite katika kutoa matokeo yatakayoweza kutatua matatizo ya wananchi na kuendelea kutengeneza ajira ili kuinua kipato cha wananchi na uchumi wetu kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako wakati wa kuzindua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Katika Kutekeleza agizo la Uchumi wa viwanda tunategemea rasilimali watu yenye ufahamu, ujuzi, teknolojia na ubunifu ili kuzalisha kwa tija na kuhimili ushindani wa kimataifa.
Profesa Joyce amesema kuwa Tafiti zilenge katika kuimarisha uchumi wa viwanda zikiwa ni muhimu katika kuinua tija na uzalishaji,
“Baadhi ya tafiti za Kilimo zilizofanywa na taasisi zetu kama vile Chuo Kikuu cha Sokoine zimefanikiwa kutoa matokeo mazuri. Hii inajumuisha mbegu bora zinazoongeza mavuno kama vile mbegu za mihogo, mahindi na mpunga ambazo zinavumilia ukame na zinaweza kukinzana na magonjwa”. Amesema Profesa Joyce.
Aidha amewaomba wakamilishe mapema taratibu zinazohitajika ili watanzania wengi waweze kunufaika na chanjo hizo muhimu kwa wafugaji wa kuku.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Dkt. Hassan Mshinda amesema kuwa tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeweza kupata chanjo inayozuia magonjwa ya kuku kama vile mdondo, ndui na mafua katika chuo Kikuu cha Sokoine .
No comments
Post a Comment