Picha kwa msaada wa mtandao |
Na John Banda, Dodoma
NAIBU waziri
wa TAMISEMI Seleiman Jaffo amesema swala la wanafunzi hewa si jambo dogo
bali ni jambo ambalo limekuwa likifanywa na watumishi wasio waamifu kwa muda mrefu sasa katika
idara ya Elimu ambapo kutokana na hilo Serikali imetoa maelekezo kwa
wakurugenzi wote nchini kutoa idadi ya wanafunzi
Akiongea katika
kamati hiyo ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa [Tamisemi] alisema kwa sasa Serikali
inatoa 18.7.7 Bilion kwa ajili ya kugalimia Elimu Bure
Jaffo
alisema kuwa kitendo hicho cha uwepo wa wanafunzi hewa ni mchezo ambao
umezoeleka kwa kuwa imegundulika kuwa umekuwa ukifanywa tangu zamani ambapo kwa serikali hii hauwizi kuendelea
Alisema kuwa
hivi sasa serikali imeshatoa maagizo kwa mikoa na halmashari zote nchini kwa
wakurugenzi kupeleka taarifa ya wanafunzi waliyopo shuleni kiasi cha fedha
zilizotumika kuwahudumia ambayo itasaidia kudhibiti Fedha za serikali
“lengo letu ni kuwa tunapotoa mgao wa fedha kwa kila shule zitosheleze mahitaji ya kuhudumia kila mwanafunzi,
kwa sasa kila mwalimu anapokea Fedha za kuhudumia wanafunzi wa shule yake Katika hili
tumejiapanga kuwahudumia watanzania na hivyo kila kitu kitaenda sawa” alisema
Aidha Jaffo
alikiri kuwa hivi sasa kuna tatizo kubwa la upungufu wa walimu hasa wa sayansi
na hisabati ambapo kutokana na hilo wanategemea rais
atakaporidhika kutokana na uchunguzi aliokuwa akiufanya tatizo hilo litamalizwa
kwa awali ilionekana walimu wengi wanaajiliwa kwa utaratibu usiofaa.
“leo
tumekutana na kamati ya tamisemi na mtazamo wao mkubwa ni huo kuhusu upungufu
wa walimu lakini niseme tu kuwa Rais alisimamisha mchakato wa ajira ili kupisha
uchunguzi lakini mara atakaporidhika mambo yote yatakuwa sawa”, alisema
aliongeza
kuwa hata upandishaji wa madaraja ya walimu mtindo uliokuwa ukitumiwa
ni wa hongo ya ngono na ndiyo sababu ilifika wakati wakilinganishwa
walimu wenye vyeo na wasio na vyeo kulikuwa na utofauti kwa wasio na
vyeo ndio walikuwa na uwezo wa kufanya kazi kiueledi kuliko wakubwa wao
alisema
tayari serikali imeshaunda tume ya kulifuatilia hilo na kuhakikisha
walimu wote watakaopandishwa vyeo ni wale wanaostahili na si vinginevyo
No comments
Post a Comment