Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » SERIKALI KUANDAA MATAMASHA MBALIMBALI ILI KUTOA ELIMU JUU YA KURIDHIWA KWA MKATABA WA MATUMIZI YA DAWA NA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo pamoja na  Tume ya Taifa ya UNESCO wamekusudia kuandaa matamasha na matembezi mbalimbali ili kutoa elimu kwa jamii kuhusu udhibiti wa matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo,  Dkt. Moshi Kimizi namna ambavyo Serikali imekusudia kuanzisha kampeni hizo ili kuionyesha jamii athari mbalimbali za kisaikolojia na kiafya kwa wachezaji na hasa vijana.
Aliongeza kuwa mwezi Juni mwaka huu, Bunge la Tanzania liliridhia mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu katika michezo, hatua iliyolenga kulinda na kuimarisha afya za wanamichezo nchini.
“Kwa kuridhia mkataba huu na kuutekeleza itainufaisha nchi kuweza kuhudhuria mafunzo, mikutano na vikao vya kimataifa na kushiriki katika makongamano yenye maamuzi mbalimbali yanayohusu suala hili” alisema Dkt. Kimizi.
Kwa mujibu wa Kimizi alisema kupitia mkataba huo, wanamichezo, walimu wa michezo na wadau wa michezo wataweza kuelimishwa kuhusu athali za matumizi ya dawa au mbinu za kuongeza nguvu michezoni pamoja na aina ya vyakula au vinywaji ambavyo vina asili ya kuongeza nguvu mwilini.
Kwa upande wake Afisa Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Rashidi Mijuza alisema  kuwa, wanamichezo wengi hujikuta wakiwekewa dawa za kuongeza  nguvu na walimu wao katika chakula au vinywaji bila kujua ili tu waweze kushinda.
Kwa mujibu wa Mijuza alisema Serikali imekusudia kutoa elimu kwa wanamichezo na walimu ili kuondokana na visingizio vya kutojua au udanganyifu ambao umekuwa ukifanyika kwa wanamichezo pindi wanapokuwa katika mashindano mbalimbali.
“Kwa Tanzania kuridhia mkataba huo, nchi itanufaika na mambo mbalimbali katika sekta ya michezo ikiwa ni pamoja na Tanzania kushiriki na kuandaa mashindano mbalimbali ya kimataifa, kupata misaada ya wataalamu, fedha na mafunzo kwa ajili ya utekelezaji wa makubaliano” alisema Mijuza

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / SERIKALI KUANDAA MATAMASHA MBALIMBALI ILI KUTOA ELIMU JUU YA KURIDHIWA KWA MKATABA WA MATUMIZI YA DAWA NA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI.

No comments :