Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

Msanii Hussein Machozi ambaye sasa amerudi nchini kutoka nchini Italia amefunguka na kusimulia kisa chake cha kufumaniwa alivyokuwa Kenya na kusema kuwa kama asingekimbia huenda mambo yangekuwa mabaya kwake.

Hussein Machozi amesema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa yeye alikwenda Kenya kikazi na mtu ambaye alikuwa anawasiliana naye alikuwa ni binti aliyeandaa show yake Kenya, hivyo alipofika alimpokea Airport na kwenda naye hotel.

"Kwa hiyo tulipofika hotel tulikuwa tunapanga mipango ya hapa na pale, kumbe yule binti ana mshikaji wake ambaye ana wivu sana na yeye, hivyo yule jamaa alikuja na magari kama mawili yakiwa na mabaunsa kibao.

"Wakatuzunguka pale na kuanza kunipiga vibao ila nashukuru Mungu kuna baunsa mmoja pale pale alinishtua na kuniambia nikimbie, hivyo niliruka ukuta wa hotel na kukimbia. 

"Kwa hiyo wale wahudumu pale ndiyo walianza kusambaza habari kuwa nimefumaniwa ila nisingekimbia huenda ingekuwa mbaya kwangu"alisisitiza Hussein Machozi 

Mbali na hilo Hussein Machozi anasema alimua kwenda nchini Italia baada ya kuona muziki unampa mawazo hivyo Mungu akamfungulia mlango  mwingine na kuamua kusepa huko, ambako anadai anasoma na kufanya shughuli zingine zinazomuingizia kipato.

Baada ya kuenea uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa mchekeshaji MC Pilipili anatoka kimapeniz na Rose Ndauka, muigizaji huyo amekanusha uvumi huo.

Wiki chache zilizopita kupitia kipindi cha The Play List cha Times FM mchekeshaji huyo alidaiwa kukiri kutoka kimapenzi na muigizaji huyo.

Jana ijumaa muigizaji huyo amescreenshot ujumbe wa mtangazaji wa The Play List, Lilommy ambao ulidai huwenda wawili hao wakawa wanatoka kimapenzi na kuandaika

 “Jamaniii naomba niweke ili swala sawa sawa, mimi na MC Pilipili ni watu tunaofahamiana haswa kwenye kazi hatuna uhusiano wowote wa kimapenzi. NADHANI NTAKUWA NIMEELEWEKA”

Msanii wa Bongofleva ambaye anafanya vizuri kwa sasa kutokana na kuachia hit-songs kila kukicha na kuteka muziki wa Africa, Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii waliopewa heshima ya kufanya show katika tuzo ya mchezaji bora Africa January 5 na michuano ya mataifa ya Afrika 2017.

Diamond ataanza kuperform katika utoaji wa tuzo za mchezaji bora Afrika kwa mwaka 2016 maarufu kama CAF Glo Awards ambazo zitafanyika January 5 Nigeria, ila January 14 2016 ataperform katika uwanja wa Stade de l’AmitiĆ© Libreville wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 40000 wa kabla ya mchezo wa ufunguzi kati ya mwenyeji Gabon dhidi ya Guinea-Bissau.

Gazeti la Kenya liitwalo taifa leo limeripoti kwamba bodi ya filamu kwenye nchi hiyo imehuzunishwa na Msanii wa muziki wa Injili SBJ kuimba wimbo wa Injili ambao unadhalilisha Imani.

Wimbo wenyewe unaitwa ‘Yesu nipe nyonyo‘ ambapo mkuu wa bodi hiyo Ezekiel Mutua alisema baadhi ya Waimbaji wa Kenya wamekosa maadili na kipaji cha kubuni au kutunga nyimbo nzuri zisizochafua hali ya hewa.

Alisema wimbo huo unaendelea kukaguliwa kwa sababu Wakenya wamekasirishwa: "Nashangaa sana mtu mzima anakaa chini na kuimba wimbo kama huu, Wasanii wetu wamejua kuwa kama hawaongei uchafu ama kutoa video za utata hawatasikilizwa wala kutazamwa na wanafanya hivyo ili wapate umaarufu”

Tayari bodi hiyo ilikua kwenye mipango ya kuwaandikia Youtube ambao ndio wanamiliki wa mtandao huo ili waiondoe hiyo video kwasababu bodi hiyo inayo mamlaka na katiba haitakubali Wasanii kutunga nyimbo za kudhalilisha imani.

Mpaka sasa wimbo huo bado upo kwenye mtandao na umeshatazamwa mara 93,812 mpaka sasa.

HATIMAYE staa wa muda wote katika muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ a.k.a Jide leo amekiri bila kupepesa maneno kuwa yupo katika penzi zito na mwanamuziki mwenzake raia wa Nigeria aitwaye Chris maarufu kama Spicy a.k.a Rasta.Jide ameyafunguka hayo wakati akifanya Exclusive Interview na Global TV Online kwenye studio zake zilizopo ndani ya Ofisi za Global Publishers Ltd eneo la Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mbali na kuwa katika mahaba na Rasta, Jide amefunguka kuwa tayari wana project ambayo anaifanya na mpenzi wake huyo na inatarajiwa kuwa mtaani kesho Jumatano ya Desemba 14, 2016.
Global TV Online ilimtupia swali mpenzi wa Jide ikimuuliza kuwa ni wapi alikutana na mrembo huyo, na haya ndiyo yalikuwa majibu ya Rasta.
“Aaah, i can’t explain it here, but i didn’t meet Jide in Tanzania” akimaanisha kuwa hawezi kuelezea kuhusu mahusiano yake na Jide lakini hakukutana naye hapa Tanzania.
Jide kwa upande wake anasema alikutana na Rasta katika kazi zao za muziki maana wote ni wasanii kama ambavyo wafanyakazi wa benki wanaweza kuingia katika mapenzi kwa kuwa wote wapo karibu kikazi.
Spicy alipoulizwa ni mpango gani anao na dada yetu alisema wanapendana na mambo mengine yatajulikana kadri muda unavyokwenda.
Kuhusu tuzo aliyoipata juzi katika EATV Awards 2016 ya Mwanamuziki Bora wa Kike, Jide alisema amejisikia vizuri na imemtia nguvu katika kazi yake ya muziki.
Global TV Online ilimtupia swali lingine Jide kuhusu mbinu gani aliyotumia kumchunguza mpenzi wake huyo, ambapo alisema hakutumia muda mwingi kumjua na kwamba walipokutana walijikuta wamezama katika mapenzi hivyo haikumchukua muda mrefu kufikiria hilo.
Chanzo:GPL

Aliyekuwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali na Wakili nchini Afrika Kusini Thuli Madonsela leo ametangazwa kuwa ndiye mshindi  wa Tuzo ya Mtu Mashuhuri Afrika ya Forbes (Person of the Year #POY2016).

Tuzo huyo hupewa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuiinua jamii kwenye njanja mbalimbali za maisha kama vile uchumi, siasa, utamaduni.

Katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo, Thuli Madonsela alikuwa akichuana na Michiel Le Roux kutoka Afrika Kusini, Rais wa Mauritania, Ameenah Gurib, Jamii ya watu wa Rwanda na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

BURUDANI