JAMHURI
YA KIDEMOKRASIA YA KONGO
Wakazi wa eneo la mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameomba kuzidishwa idadi ya wanajeshi katika
eneo hilo ili kuwalinda.
Wakazi wa eneo la Shabunda katika
mkoa wa Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameiomba
serikali ya nchi hiyo iongeze idadi ya wanajeshi katika eneo hilo.
Drid Bambabwenge Msemaji wa wakazi
wa eneo la Habunda ameeleza kusikitishwa na jinai zilizofanywa na wanajeshi kwa
jina la "Raia Mutomboki" khususan katika barabara ya
Burhale-Shabunda.
Bambabwenge amewatuhumu wanamgambo
wa "Raia Mutomboki" kwa kuwapora, kuwateka nyara na kufanya
mashambulizi ya kuvizia dhidi ya raia.
Hii ni katika hali ambayo eneo la
mashariki mwa Kongo tangu miaka 20 iliyopita hadi sasa limeathiriwa na
machafuko kufuatia kuwepo makundi ya waasi.
Eneo hilo linaendelea kuathiriwa na
machafuko kufuatia kushindwa jeshi la Kongo na wanajeshi wa kofia bluu wa Umoja
wa Mataifa kuwaangamiza wanamgambo hao.
MAREKANI
Mgombea wa Democratic Hillary
Clinton na mgombea wa Republican Donald Trump wameshinda majimbo mengi katika
mchujo wa kuteua wagombea urais Marekani katika vyama vyao Jumanne Kuu.
Wagombea wote wawili wameshinda
majimbo saba kila mmoja. Wameshinda wote wawili majimbo ya Alabama, Georgia,
Tennessee na Virginia.
Bi Clinton pia ameshinda Arkansas na
Texas, naye Bw Trump akashinda Massachusetts.
Bw Trump hata hivyo ameshindwa na
Seneta Ted Cruz majimbo ya Texas, Alaska na Oklahoma.
Mgombea wa Democratic Bernie Sanders
naye ameshinda kwake nyumbani katika jimbo la Vermont, Minnesota, Colorado na
pia katika jimbo la Oklahoma.
Mchujo wa Jumanne Kuu hushuhudia
majimbo 11 yakifanya mchujo kwa pamoja huku maandalizi ya uchaguzi mkuu tarehe
8 Novemba yakiendelea kushika kasi.
Bi Hillary Clinton, aliyekuwa wakati
mmoja waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, pamoja na mfanyabiashara tajiri
kutoka New York Donald Trump walipigiwa upatu kushinda majimbo mengi Jumanne
Kuu.
Utafiti wa maoni ya baada ya kura
ulikuwa umeonyesha Trump na gavana wa Ohio John Kasich wakikabiliana vikali
katika mchujo wa chama cha Republican jimbo la Vermont, lakini baadaye Trump
aliibuka mshindi.
Bi Clinton na Bw Sanders pia
walikabiliana vikali katika jimbo la Massachusetts, kaskazini mashariki mwa
Marekani lakini Clinton akaibuka mbabe.
Bbcswahili.com
UGANDA
Forum for
Democratic Change - FDC - ambacho mshika bendera wake Dr Kiiza Besigye bado
anazuiliwa nyumbani kwake na vikosi vya usalama kimetoa masharti kadhaa ili
kutuliza hali ya kisiasa ambayo inaendelea nchini Uganda tangu matokeo ya
uchaguzi wa Febuari 18.
FDC kimetaka vikosi vya usalama
kuacha kuzingira sio tu nyumba na mshika bendera wake lakini pia na ofisi zao.
Mkuu wa chama hicho, Meja Jerali
Mustaafu Mugisha Muntu, mbele ya waandishi habari katika makao ya chama hicho
mtaa wa Najanankubi mjini Kampala ametaka serikali itoe mzingiro katika nyumba
ya Dkt Kizza Besigye.
FDC inadai kuwa wafuasi wake zaidi
ya 300 baadhi wakiwa mawakala wamekuwa wakikamatwa kiholela nchini kote.
Aidha kinashuku matokeo ya uchaguzi
ambayo yalitangazwa na tume ya uchaguzi iliompa ushindi Museveni, huku Meja
Jenerali Mugisha akitoa sababu ya kuunda kwa tume hiyo.
Hata hivyo amepinga wazo la kutumia
mabavu kufikia malengo yao akisema kuwa hiyo sio njia yao.
Bbcswahili.com
ZIMBABWE
Gazeti la
serikali - Herald - linaariifu kuwa waendesha mashtaka wamewarudishia mashtaka
wanajeshi wawili wanaotuhumiwa kulilipuwa kwa bomu la petroli shamba la maziwa
linalomilikiwa na familia ya rais Robert Mugabe.
Linaarifu kwamba, hatua hiyo
inakiuka uamuzi wa mwendesha mashtaka mkuu kutupilia mbali mashtaka hayo dhidi
ya wanajeshi hao wenye umri wa miaka ya 29 na 37.
Mawakili wa wanajeshi hao
wanashinikiza kesi itupiliwe mbali wakieleza kuwa haiwezekani kwa Tomana
kugeuza kauli yake na kuamuru washtakiwe.
Herald imeripoti, mawakili wa
serikali wanasema naibu wa Tomana alichukua uamuzi huo wa kuwashtaki upya
wanajeshi hao baada ya kufuata sheria zinazazohitajika.
Tomana ameachiliwa kwa dhaman baada
ya uamuzii wake kumsababisha kushtakiwa kwa kuzuia sheria itendeke.
Amekana mashtaka.
Bbcswahili.com
Kundi la kimataifa la wanasayansi lilichukua violezo vya DNA vya takriban watu 6000 waliojitolea kutoka Ulaya,Marekani na Waafrika.
Jeni hiyo aina ya IRF4 husimamia nywele za kawaida,ngozi na rangi ya macho inayoitwa Melanin.
Mwanasayansi kutoka katika chuo cha London alisema:tayari tunajua jeni kadhaa zinazozohusishwa na kumea kwa upara, na rangi ya nywele na jeni zinazosababisha umbile la nywele.
Bbcswahili.com
No comments
Post a Comment