Viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wameidhinisha kwa
kauli moja Sudan Kusini kujiunga na jumuiya hiyo. Uamuzi huo
umechukuliwa na viongozi hao kwenye mkutano wao uliofanyika mjini
Arusha, Tanzania leo Jumatano.
Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki imesema
viongozi wameridhia Sudan Kusini kuwa mwanachama wa 6 wa EAC baada ya
kutimiza masharti yote yanayohitajika kwa mwanachama mpya.
Mkataba uliopelekea kuundwa Jumuiya ya Afrika Mashariki unasema kuwa, ili nchi ikubaliwe kuwa mwanachama ni sharti iwe inaheshimu misingi ya demokrasia, haki za binadamu, usawa wa jamii, utawala bora, uwazi na uwajibikaji.
Sudan Kusini iliomba kujiunga na EAC punde baada ya kujitangazia uhuru wake kutoka kwa Sudan mwaka 2011. Hata hivyo, mchakato wa kuiidhinisha nchi hiyo umekuwa ukisuasua kutokana na kile kilichotajwa kuwa ni udhaifu kwenye taasisi muhimu za nchi hiyo pamoja na hali mbaya ya usalama.
Kwa kuidhinishwa Sudan Kusini kuwa mwakachama wa 6 wa EAC, kumuiya hiyo sasa imekuwa na idadi jumla ya watu milioni 162.

No comments
Post a Comment