Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » JITIHADA ZA SERIKALI KUBORESHA SEKTA YA MIFUGO.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

SERIKALI ya Awamu ya Nne inaondoka madarakani ikiwa na mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi ya sekta ya mifugo na ufugaji kama ilivyoanishwa kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015.
Sekta ya mifugo na uvuvi ni miongoni mwa vipaumbele vilivyowekwa na Awamu ya Nne ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kutekeleza ilani yake ya kuhakikisha wafugaji wanaingia kwenye ufugaji wa kisasa ili kutunza mazingira na kuongeza mazao yanayotokana na ufugaji kwa manufaa ya wafugaji na taifa kwa ujumla. Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ilipoingia madarakani mwaka 2005 ilielezea dhamira yake ya kufanya mageuzi katika sekta mifugo ili kuongeza uzalishaji na kuimarisha maisha ya wafugaji.

Pamoja na changamoto mbalimbali katika sekta hiyo serikali imefanikiwa kutekeleza azma yake kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Mifugo yenye lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo hasa maziwa, nyama na mayai. Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani anasema baada ya Serikali ya Awamu ya Nne kuingia madarakani imeanzisha na kutekeleza wa programu ya uzalishaji wa mazao ya mifugo hasa maziwa, nyama na mayai.
Programu hiyo imepata mafanikio makubwa ambapo uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita bilioni 1.4 mwaka 2005 hadi lita bilioni 2.06 mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia 47. Idadi ya ng’ombe bora wa maziwa imeongezeka kutoka 510,000 mwaka 2005 hadi kufikia 780,000 mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la asilimia 52. Pia uzalishaji wa nyama umeongezeka kutoka tani 378,509 mwaka 2005 hadi tani 597,757 mwaka 2015, sawa na ongezeko la asilimia 58.
Vilevile, unenepeshaji wa ng’ombe umeongezeka kutoka ng’ombe 62,000 mwaka 2008 hadi ng’ombe 213,000 Februari mwaka 2015. Unenepeshaji wa ng’ombe unafanyika katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Arusha, Rukwa, Tabora, Tanga, Pwani na Kilimanjaro. Kamani anasema uzalishaji wa mayai umeongezeka kwa asilimia 133 kutoka mayai bilioni 1.8 hadi mayai bilioni 4.2 katika mwaka 2015.
Pia uzalishaji wa vifaranga vya kuku wa nyama na wa mayai umeongezeka kutoka vifaranga milioni 26.8 hadi milioni 64 mwaka 2015. Pia mashamba makubwa ya kuzalisha vifaranga yameongezeka kutoka mashamba 10 mwaka 2005 hadi mashamba 21 Februari mwaka huu 2015. Mradi wa kopa ng’ombe lipa ng’ombe Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2005 hadi Februari 2015, Serikali imesambaza jumla ya mitamba 70,862 na mbuzi wa maziwa 13,517 kupitia Mpango wa kopa ng’ombe lipa ng’ombe pia kopa mlipa mbuzi katika mikoa yote nchini.
Mashamba ya kuzalisha mifugo ya Sao Hill, Nangaramo, Kitulo, Ngerengere na Mabuki yameimarishwa kwa kukarabati nyumba 40 za watumishi na kupatiwa vitendea kazi kama vile magari, matrekta na zana zake pamoja na mashine za kukamulia. Vilevile, mashamba hayo yalipatiwa jumla ya ng’ombe wa maziwa 3,495 na madume 230. Udhibiti wa magonjwa ya mifugo Serikali imeendelea na jitihada za kudhibiti magonjwa ya mifugo ikiwemo ugonjwa wa homa ya mapafu ya ng’ombe.
Jumla ya dozi milioni 25.7 za chanjo zenye thamani ya Sh bilioni 2.93 zimetumika kuchanja ng’ombe milioni 24.4 katika mikoa ya Pwani, Tabora, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Singida, Iringa, Mbeya na Rukwa. Pia serikali imeendelea kutoa ruzuku ya dawa za kuogeshea mifugo ambapo hadi Februari 2015 jumla ya Sh bilioni 20.3 zimetolewa kama ruzuku na kununua jumla ya lita milioni 1.32 za dawa za kuogesha mifugo kwa mikoa yote Tanzania Bara.
Kutokana na juhudi hizo, vifo vya ndama vimepungua kutoka wastani wa asilimia 40 hadi chini ya asilimia 10 katika maeneo yaliyozingatia taratibu za uogeshaji. Aidha, udhibiti wa ugonjwa wa ndigana kali ya ng’ombe kwa njia ya chanjo umeendelea kufanywa ambapo ng’ombe 810,000 walipatiwa chanjo ya kinga na kupunguza vifo vya ndama kutoka asilimia 85 hadi asilimia 5. Ujenzi wa mabwawa na majosho Serikali kupitia Mipango ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Wilayani na Sekta Binafsi, imejenga malambo 1,008, majosho 2,364, maabara 104 za mifugo na visima virefu 101.

Aidha, Serikali imekarabati jumla ya malambo 370, majosho 499 na hivyo kuongeza idadi ya majosho kutoka 2,177 hadi 3,637. Kuwepo kwa malambo kumewezesha mifugo kupata maji hususan wakati wa kiangazi pamoja na kupunguza uhamaji wa wafugaji na migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi. Utafiti wa mifugo na huduma za ugani Serikali imeanzisha wakala wa mafunzo ya mifugo kwa lengo la kuboresha na kuimarisha mafunzo ya wataalamu wa mifugo.
Wakala huo una kampasi 8 ambazo ni Morogoro, Tengeru, Mpwapwa, Buhuri, Madaba, Temeke, Kikulula na Mabuki. Aidha, idadi ya wanachuo wanaodahiliwa katika vyuo vya mafunzo ya mifugo katika ngazi za astashahada na stashahada imeongezeka kutoka 738 kwa mwaka katika mwaka 2005/2006 hadi 2,451 kwa mwaka katika mwaka 2014/2015.
Vilevile, katika kipindi cha miaka 10, Serikali imeongeza ajira za wagani wa mifugo katika halmashauri mbalimbali nchini kutoka 2,270 mwaka 2005 hadi kufikia 8,541 mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia 276. Jumla ya vikundi 1,820 vya wafugaji vimeundwa na vinajihusisha na ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa katika mikoa ya Mbeya, Arusha na Tanga.
Pia uboreshaji ng’ombe wa asili unafanyika katika Morogoro, Dodoma, Mwanza na Shinyanga). Programu ya ufugaji wa mbuzi wa maziwa unafanyika katika mikoa ya Arusha na Manyara, kuku wa asili katika mikoa ya Dodoma na Singida na ufugaji wa kuku wa kisasa katika mikoa ya Morogoro na Mwanza. Pia ufugaji wa kondoo unafanyika katika Arusha na Manyara, udhibiti wa ndorobo katika mkoa wa Tanga, ufugaji wa nguruwe unafanyika katika mkoa wa Rukwa na Mbeya wakati programu maalumu ya ufugaji wa sungura unafanyika katika Morogoro na Mtwara.
Masoko ya ndani ya mifugo na mazao yake Serikali imeanzisha mkakati wa kufufua na muendeleza sekta na viwanda vya ngozi unaotekelezwa katika halmashauri 75 za mikoa 18 kwa kutumia fedha za mfuko wa maendeleo ya mifugo. Utekelezaji wa mkakati huo umesaidia kuongeza usindikaji wa ngozi unaofanyika nchini kutoka vipande 790,000 vyenye thamani ya Sh bilioni 1.9 mwaka 2005 hadi vipande milioni 3.78 vyenye thamani ya Sh bilioni 71.5 mwaka 2014.
Jumla ya wafugaji 6,047, wachinjaji na wachunaji 4,285 wamepatiwa mafunzo kuhusu mkakati wa kufufua na kuendeleza sekta ya viwanda vya ngozi nchini. Pia jumla ya machinjio 67 yamefanyiwa ukarabati. Hatua hizo zimeongeza ubora na thamani ya ngozi pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania. Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na kuhamasisha sekta binafsi kujenga viwanda na machinjio ya kisasa katika maeneo mbalimbali nchini.
Viwanda na machinjio hayo ni pamoja na ‘Sumbawanga Agricultural and Animal Feeds Industries’ kilichopo Iringa, Chobo kilichopo Mwanza, Triple S Tandani Mkuranga, Kiliagro cha mkoani Arusha, Mtanga Foods Limited (Kilolo), Alpha Choice kilichopo Magu, ORPUL (Simanjiro), Xinghua International (Shinyanga) na Engahay Babati mkoani Manyara. Idadi ya viwanda vya kusindika maziwa imeongezeka kutoka 22 hadi 74 kati ya mwaka 2005 na 2014.
Uwezo wa usindikaji wa maziwa kwa siku pia umeongezeka kutoka lita 56,580 mwaka 2005 hadi lita 139,800 Februari, 2015 sawa na ongezeko la asilimia 147. Vituo 22 vya kukusanyia maziwa vimejengwa katika mikoa ya Arusha, Mara, Tanga, Iringa, Manyara, Kilimanjaro, Morogoro, Rukwa, Kagera na Mwanza. Pia, matangi matatu ya kupoza maziwa yamepelekwa katika vyama vya wafugaji Siha, Njombe na Pongwe (Tanga) ili kuongeza ukusanyaji na usindikaji wa maziwa.
Vituo vya kuzalisha mbegu bora za mifugo Serikali imeongeza vituo vya uhamilishaji kutoka kituo kimoja cha Arusha mwaka 2005 hadi kufikia vituo nane Februari mwaka 2015 ambavyo vipo katika Mikoa ya Mbeya, Katavi, Mwanza, Pwani, Dodoma, Lindi na Sao Hill (Iringa) kinachoendelea kujengwa. Serikali imetoa dozi 755,584 za mbegu bora zimezalishwa na kusambazwa kwa wafugaji na ng’ombe 955,360 wamehamilishwa.
Vilevile, wataalamu 1,378 kutoka maeneo mbalimbali wamepata mafunzo ya uhamilishaji. Serikali kupitia NARCO imetenga vitalu 124 vya ufugaji ambapo vitalu 96 vimemilikishwa kwa wawekezaji binafsi ambao wameviimarisha kwa kujenga miundombinu ya maji, malisho, majosho, nyumba za watumishi na ofisi. Hadi kufikia mwaka 2014, jumla ya ng’ombe 36,820, mbuzi na kondoo 8,612 waliwekezwa katika vitalu hivyo.
Wawekezaji Watanzania 400 walipata ushauri na mafunzo ya kusimamia ufugaji wa kisasa kutoka Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO). Katika kipindi hicho, jumla ya ng’ombe 72,182 wameuzwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa ambapo kati ya hao ng’ombe 21,635 walinenepeshwa. Kutenga maeneo ya malisho ya mifugo Serikali imeendelea kuhimiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kutenga ardhi kwa ajili ya shughuli za ufugaji kwa kuzingatia mipango ya matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji kote nchini.
Kutokana na jitihada hizo, maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za ufugaji yameongezeka kutoka hekta 930,279 mwaka 2005 hadi hekta milioni 1.95 mwaka 2015. Maeneo hayo yapo katika mikoa 22, wilaya 81 na vijiji 620.
Aidha, Serikali imechukua hatua za kuhamasisha ufugaji wa kisasa ikiwa ni pamoja na kuanzisha na kuvijengea uwezo vituo vya uzalishaji wa mbegu bora za malisho katika mashamba ya Vikuge (Kibaha), Langwira (Mbarali), Mabuki (Misungwi), Buhuri (Tanga), Kizota (Dodoma Manispaa), Kongwa (Kongwa), Mivumoni (Muheza) na Sao Hill (Mufindi).
Uzalishaji wa mbegu bora za malisho kwenye mashamba hayo umeongezeka kutoka tani 15.7 mwaka 2005 hadi tani 48.5 Februari mwaka 2015. Vilevile, uzalishaji wa hei katika mashamba ya Serikali umeongezeka kutoka marobota 109,000 mwaka 2005 hadi 500,000 Februari mwaka juu. Wazalishaji binafsi wa malisho bora wameongezeka kutoka wawekezaji sita mwaka 2005 hadi 40 Februari mwaka 2015 ambapo uzalishaji wa hei kwenye mashamba ya wawekezaji umeongezeka kutoka marobota 69,100 mwaka 2005 hadi 457,860 mwaka 2015.
Uzalishaji wa vyakula vya mifugo Serikali imeendelea kuhamasisha sekta binafsi kushiriki katika uzalishaji wa vyakula vya mifugo ambapo uzalishaji umeongezeka kutoka tani 559,000 mwaka 2005 hadi tani 1,200,000 Mei mwaka 2015. Idadi ya viwanda vya kuzalisha vyakula vya mifugo imeongezeka kutoka viwanda 6 mwaka 2005 hadi 80 Februari mwaka 2015 vikiwa na uwezo wa kusindika tani milioni 1.4 za vyakula hivyo kwa mwaka.
Viwanda hivyo vipo katika mikoa ambapo ya Dar es Salaam kuna viwanda 34, Kilimanjaro viwanda sita, Mbeya viwanda vitano, Mwanza 10, Shinyanga vitatu, Singida kimoja, Dodoma kimoja, Lindi kimoja, Morogoro kimoja, Arusha saba na Pwani tisa.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / JITIHADA ZA SERIKALI KUBORESHA SEKTA YA MIFUGO.

No comments :