Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » JK AMWAGIA SIFA MAGUFULI,AMTAKA KUENDELEA NA MOTO HUO HUO
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Rais aliyeondoka mamlakani majuzi nchi Tanzania amesifu jinsi Rais mpya John Magufuli ameanza kufanya kazi na kumtaka aendelee vivyo hivyo.

Rais mstaafu Jakaya Kikwete alisema hayo wakati wa kukabidhi rasmi afisi yake kwa Rais Magufuli aliyeapishwa Novemba 5 baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25.

“Umeanza vizuri, baki na msimamo huo huo utasaidia sana wananchi,” alisema Bw Kikwete.

Dkt Magufuli amekuwa akifanya ziara za kushtukiza, ya kwanza ikiwa katika makao makuu ya Wizara ya Fedha siku yake ya kwanza kazini ambako aliwakuta wafanyakazi wengi wakiwa wametoka afisini.

Siku chache baadaye, alifanya ziara ya kushtukiza hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alisikitishwa na utoaji huduma.

Hafla ya kukabidhi rasmi afisi kwa Rais Magufuli ilishuhudiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Maafisa wa Ofisi Binafsi ya Rais.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu, Rais mstaafu Kikwete alimkabidhi Rais Magufuli taarifa rasmi yenye kurasa 53, ambayo kwa ujumla inaelezea kazi zilizokwisha kufanyika, ambazo zinasubiri kukamilika na zile ambazo zinasubiri maamuzi ya utekelezaji.

Mengine ni hali halisi ya nchi katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / JK AMWAGIA SIFA MAGUFULI,AMTAKA KUENDELEA NA MOTO HUO HUO

No comments :