Na Peter Mkwavila,Dodoma.
WAKAZI wa vijiji vya Chunyu na Nghambi wilayani Mpwapwa wamekuwa wakilazimika kuwandangaya watoto wao kwa kuwasha moto asubuhi na kuchemsha mawe kwa kuwaridisha kuwa wanapika chakula kuepuka vilio vya njaa.
Hali ambayo pia imewalazimisha kula matunda ya porini na kisamvu ili kukabiliana na njaa kali iliyopo
kwenye eneo hilo hivyo kumtaka Mbunge
wa Jimbo hilo George Lubeleje kuwasaidia kutatua tatizo hilo.
wakazi wa vijiji hivyo walisema wamekuwa wakitumia mbinu hiyo ikiwemo
na kutumia matunda ya porini yanayofahamika (Manyakfwega) ili kupunguza njaa waliyonayo.
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Nghambi Peter Mkanwa,
alisema kuwa imembidi kwenda porini kusaka matunda hayo ambayo hata hivyo
yameanza kuadimika kwa ajili ya kupunguza njaa iliyoikumba familia zilizo
nyingi.
Alisema kutokana na tatizo hilo kuwa ni kubwa kwenye
eneo hilo la vijiji,akina mama walio wengi wanatumia mbinu za kuchemsha mawe
asubuhi kwa kuyafunika kwenye sufuria hivyo wakiona vile wanajua watapata mlo
kwa siku hiyo.
“Ndugu mwana habari hapa tuna njaa ya ajabu
unavyoniona naelekea porini kutafuta matunda kwani nyumbani hakuna chakula,ila kama hata
una shilingi 500 naomba ninunue unga tukakoroge uji ili tunywe na familia
yangu’’Mkanhwa alisema.
Naye Juma Mwanamboka alimtaka Mbunge wa Jimbo hilo kuishirikisha
serikali ili iweze kulishughulikia suala hilo kwa umakini kwa kutafuta ufumbuzi
wa haraka kwani familia nyingi zimekuwa zikiadhirika.
Mwanamboka alisema kutokana na njaa hiyo hivi sasa pia
vijana wengi wa kiume katika vijiji hivyo wamekuwa wakiitumia fursa hiyo pia kuwarubuni
watoto wetu wa kike.
Alisema kwa hali hiyo kuna hatari ya kuibuka kwa mimba
wasizotarajia ikiwemo na magonjwa ya kuambukizana kama vile maambukizi ya
virusi vya ukimwi hivyo serikali iliangalie hili pia.
Naye Salome Chishome mkazi wa kijiji cha Chunyu
alisema wamekuwa wakichuma kisamfu kwenye maeneo ya makaburi ambapo hata hivyo
pia kimeanza kuadimika ili kukabiliana na tatizo la njaa.
“Hata hivyo tunamshukuru mungu hapa kwenye makaburi
yaliyo mengi kuna miti ya mihogo mingi hivyo ndio tunakitumia kama mboga na kama
chakula”alisema.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la hilo George Lubeleje,alisema
amewaagiza madiwani kulijadili suala hilo kama hoja ya dharula katika
kikao cha baraza la madiwani kitakachokaa hivi karibuni.
Pia alimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Donoti
Nhenzi kulishughulikia suala hilo akishirikiana na kamati ya maafa kwa
kuhakikisha wanalitatua tatizo hilo kwa kuwapelekea chakula.
Naye Mkuu wa wilaya hiyo,Mohammed Utaly ambaye ndiye
Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya alisema suala la ukosefu wa chakula
limekuwa ni tatizo kutokana na ukosefu wa mvua msimu uliopita.
No comments
Post a Comment