NA JOHN BANDA,DODOMA
MKOA wa Dodoma umetangaza majina ya wanafunzi watakaojiunga
na kidato cha kwanza Januari mwakani huku 19,052 wakiwa wamefaulu.
Akitangaza matokeo hayo jana,Mjini Hapa,Afisa Elimu
Mkoa wa Dodoma Juma Kaponda alisema matokeo yanaonesha ufaulu umeongezeka hadi
asilimia 54 ambapo mwaka jana ilikuwa asilimia 45.3.
Kaponda alisema wanafunzi waliosajiliwa kufanya
mtihani walikuwa 36,273 ambapo wavulana walikuwa 15,745 na wasichana 20,528.
Alisema Halmashauri yenye ongezeko kubwa la ufaulu
ni Kondoa yenye asilimia 25 ikifuatiwa na Chemba yenye asilimia 16 huku
Chamwino ikishika mkia.
‘’Kwa ujumla mwenendo wa kitaaluma katika
halmashauri za kondoa na Chemba zinaleta matumaini makubwa tangu mwaka 2014
ambapo ongezeko la ufaulu katika halmashauri hizo kuwa za kwanza kimkoa.
Kaponda alisema Halmashauri zote hazikufikia malengo
ya BRN(Matokeo makubwa sasa) ambapo hali hiyo imefanya Mkoa kubaki katika rangi
ya njano.
Pia alisema jumla ya watahiniwa 110 wavulana 45
wasichana 65 sawa na asilimia 0.3 walifanya mtihani bila ya kujua kusoma na
kuandika hii ni pungufu na mwaka 2014 ambapo walikuwa 301.
‘’Katika mtihani huu,jumla ya shule 773 zilikuwa na
watahiniwa wa mtihani wa darasa la saba idadi ni kati ya shule 757 tulizo nazo
katika Mkoa wa Dodoma shule iliyoongoza kwa ongezeko kubwa la alama ni Madaha
ya Chemba’’alisema
Alisema katika matokeo hayo somo la English Language
ndio wanafunzi walilofanya vibaya zaidi likifuatiwa na Hisabati huku Kiswahili
likiongoza kwa ufaulu likifuatiwa na Sayansi.
‘’Ufaulu huu umefanya Mkoa ushike nafasi ya 24 kati
ya Mikoa 25,nafasi hii ni mbaya kuliko mwaka jana Halmashauri zilizopanda
kinafasi ni Kondoa,Bahi na Chemba’’alisema
Kaponda alisema ufaulu kwa wanafunzi wenye ulemavu
umeongezeka kutoka asilimia 75 za mwaka jana mpaka 97 za sasa.
Mhariri mkuu: Denis Kazenzele
No comments
Post a Comment