Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege
la Air France amefutilia mbali tahadhari ya bomu iliyosababisha ndege ya
kutua Kenya kuwa ni ya uongo
- Ndege hiyo ya abiria ya Air France Boeing 777 AF463, inayohudumu kati ya Mauritius na Paris ililazimika kutua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Mombasa - Kenya baada ya kifaa kinachodhaniwa kuwa bomu kupatikana ndani ya choo cha ndege hiyo.
- Inasemekana kuwa abiria mmoja alikipata kifaa hicho chooni na akamfahamisha mhudumu mmoja wa ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria 459 na wahudumu 14.
Ndege hiyo ilitua saa sita usiku wa kuamkia leo Jumapili, huku wataalamu wa kutegua mabomu kutoka jeshi la wanamaji la Kenya wakiingia ndani ya ndege hiyo kukagua kifurushi kilicholeta taharuki.
Sasa kitengo cha ujasusi cha Ufaransa kimeanzisha uchunguzi wa kina kubaini kilichosababisha tishio hilo.
bbcswahili
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
BBCSWAHILI
INDIA
Mfungwa mchanga
zaidi katika genge la wabakaji waliopatikana na hatia ya kubaka na kuua
mwanamke mmoja mwaka wa 2012 ameachiwa huru.
Wakili wake amaeithibitishia shirika la BBC kuwa
kijana huyo ambaye alihukumiwa akiwa chini ya umri wa miaka 18 alifungwa
kwa miaka 3 ambayo inaruhusiwa kisheria.Japo hivi sasa ametimiza miaka 18 ameruhusiwa kuachiwa huru kisheria na kupewa majina mapya na hata makosa yaliyomkabili yamefutwa.
Kijana huyo ambaye hawezi tajwa ameondoka gerezani fauka ya pingamizi kutoka kwa mashirika ya wanaharakati wa maswala ya wanawake na wazazi wa mhasiriwa wa ubakaji huo.
Kwa sasa amekabidhiwa shirika linalowashughulikia wafungwa ambao hawajatimiza umri wa utu uzima kutokana na hofu kuhusu usalama wake.
Wanne kati ya watuhumiwa waliotenda makosa hayo naye wamekata rufaa huku mtuhumiwa wa tano akiripotiwa kufariki akiwa gerezani.
Mwandishi wa BBC Sanjoy Majumder aliyeko Delhi anasema kuwa wanaharakati wengi wamejaribu kuzuia kuachiliwa huru kwa mtuhumiwa huyo japo mahakama inasisistiza kuwa inafwata sheria.
Wazazi wa mhasiriwa ambaye kifo chake kilisababisha ghadhabu kote duniani wanapinga kuachiliwa huru kwa kijana huyo.
BBCSWAHILI
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Waumini hao wa kanisa katoliki la Kutus lililoko eneo la katikati ya nchi walitoroka kanisani baada ya muumini mmoja kuona kifaa kilichokuwa kimefichwa chini ya viti alipokuwa akitoa sadaka na kuwatahadharisha wenzake.
''Tulipokuwa tukienda kutoa sadaka niliona kitu kilichokuwa kinafanana kama kisanduku kidogo na nyaya ,nilihofu sana nikamweleza padri'' alisema bwana Richard Kanyuiro.
Afisa mmoja wa polisi wa utawala aliyeitwa kushuhudia alikitambua kifaa hicho kuwa ni bomu na hivyo wakawaarifu waumi waliotorokea usalama wao.
Maafisa wa usalama kutoka Nyeri na Embu waliitwa na kuwaondoa waumi wote karibu na kanisa hilo huku wakiwasubiri maafisa wenye uwezo wa kuharibu mabomu kuwasili kutoka Nairobi.
BBCSWAHILI
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Majengo 22 yameporomoka katika maeneo ya viwandani katika mji wa Shenzhen, Kusini mwa Uchina kufuatia maporomoko ya ardhi.
Hata hivyo waokoaji wanaendelea kuwatafuta watu ambao wanashukiwa kuwa wamekwama ndani ya vifusi vya majengo hayo yaliyoporomoka
Hadi kufikia sasa hakuna mtu aliyeripotiwa kufarika ijapokuwa watu 22 hawajulikani waliko.
Mbili kati ya majumba hayo yalikuwa nyumba za malazi za wafanyikazi wa ujenzi na yamkini watu wanne wametolewa ndani ya vifusi vya majengo yaliyoanguka.
Naibu mwenyekiti wa mji huo Li Yikang, amesema wanawake 5 na wanaume 17 hawajulikani waliko.
Wazima moto 1,500 wanaendelea na shughuli ya uokoaji.
Kulingana na vyombo vya habari mchanga ambao umekuwa ukichimbwa kwa muda wa miaka miwili unaaminika kuwa ulilowa na kuporomoka.
No comments
Post a Comment