Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » KIMATAIFA KUTOKA DW SWAHILI KWA LEO DISEMBA 25/ 2O15
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

IRAN

Raia 53 wa Marekani waliozuiliwa mateka nchini Iran mwaka 1979 watalipwa fidia ya dola milioni 4.4 kila mmoja. 

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuidhinishwa leo kwa mswada wa matumizi ya pesa nchini Marekani. Wamarekani hao walizuiliwa mateka siku 444, na kisa hicho kilipelekea Marekani kukatiza uhusiano wake na Iran.

Uamuzi wa kuwalipa fidia umefikiwa baada ya makubaliano yaliyyotiwa saini kati ya nchi zenye nguvu zaidi duniani na Iran kuhusu mpango wake wa kinyuklia. 

Raia hao wa Marekani wamepigania fidia kwa miaka mingi lakini mwafaka uliopelekea kuachiliwa kwao ulikuwa na kifungu cha kuwazuia kuwasilisha madai ya fidia. 

Sheria hiyo mpya inatoa fursa ya kulipwa dola 10,000 kwa kila siku ambayo mateka alizuiliwa. wabunge wa Marekani wamesema waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea katika balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 pia watalipwa fidia.  

GEORGIA

Waziri wa mambo ya nje wa Georgia Georgy Kvirikashvili ameteuliwa kuchukua wadhifa wa Waziri mkuu hii leo baada ya Irakyl Garibashvili kujiuzulu wiki hii. 

Kvirikashvili mwenye umri wa miaka 48 ambaye pia ni naibu wa kwanza wa Waziri mkuu, ameungwa mkono na chama tawala kuchukua wadhifa huo wa Waziri mkuu. 

Uteuzi wake utawasilishwa kwa Rais na kuidhinishwa rasmi na bunge. Akiidhinishwa, Kvirikashvili ataliteua baraza jipya la mawaziri. 

Garibashvili hakutoa sababu za kujiuzulu kwake lakini wanasiasa wa upinzani wamesema ni kutokana na kushuka kwa umaarufu wa chama chake cha Georgian Dream kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Oktoba mwaka ujao. 

Upinzani unailaumu serikali kwa kudorora kwa uchumi wa taifa hilo lenye idadi ya raia milioni 3.7. 

UJERUMAN

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amekataa wazo la kupelekwa wanajeshi wa ardhini wa Ujerumani kushiriki katika mapambano dhidi ya kundi la itikadi kali la Dola la Kiisilamu IS nchini Syria.  

Kwa sasa Ujerumani inajihusisha kijeshi katika mashambulizi ya angani kulilenga kundi hilo. 

Steinmeier ametoa kauli hiyo katika mahojiano na chombo kimoja cha habari ambapo alitetea hatua ambazo Ujerumani imechukua hadi sasa kuhusiana na mgogoro huo wa Syria. 

 Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani alitetea uamuzi wa taifa hili kujihusisha kijeshi katika mgogoro wa Syria na kusema hatua hiyo ni muhimu ili kulinda usalama wa taifa la Ujerumani na watu wake. 

 Aliongeza kuwa kitisho cha kundi hilo la Dola la Kiisilamu hakina madhara tu kwa mataifa jirani bali pia  ni hatari kwa usalama wa Ujerumani hivyo wanapaswa kuchukua mapema hatua za tahadhari.

Hatua ya Ujerumani kujihusisha kijeshi katika jitihada za kuliangamiza kundi hilo la kigaidi zinafuatia mashambulizi ya Novemba 13 ya mjini Paris, Ufaransa.   

SYRIA

Shirika la kutetea haki za binadamu Syria limesema mashambulizi ya angani yaliyofanywa na majeshi ya utawala wa Syria yamewaua raia 28 wakiwemo watoto kumi karibu na mji mkuu wa Syria, Damascus. 

Takriban raia wengine 60 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo yaliyofanywa katika maeneo ya Hammuriyeh na Irbin, mashariki mwa Ghouta ambayo ni ngome kubwa ya waasi katika jimbo la Damascus. 

Mkurugunezi wa shirika hilo la kutetea haki za binadamu Rami Abdel Rahman amesema eneo hilo hushambuliwa mara kwa mara na wanajeshi wa utawala wa Rais Bashar la Assad. 

Raia wawili pia wameuawa katika eneo la Douma kaskazini mashariki mwa Damscus. 

ITALY

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amewashauri waumini wa Kristo kutopenda anasa na kujilimbikizia mali  katika msimu huu wa kupeana zawadi, na badala yake kukubali maadili ya maisha ya kawaida na yenye uwiano. 

Papa Francis kupitia hotuba yake ya kila mwaka ya Misa ya Mkesha wa Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Vatican, amewataka Wakristo kila mahali kupunguza mambo mengi ya jamii ya kisasa, ambayo amesema imechafuliwa sana na tamaa ya ulaji na raha, kupenda mali na ubadhirifu, mwonekano na kujipenda kupita kiasi na kuhimiza sikukuu ya Krismasi iwe ni wakati mwingine wa kujitambua na kujitafakari. 

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki pia alizungumzia mgogoro wa mamilioni ya wahamiaji, wakimbizi hasa wanaotoka Syria wakitafuta maisha bora Ulaya. 

Baadaye leo Ijumaa, atatoa ujumbe wa kila mwaka wa Krismasi katika Kanisal la Mtakatifu Petro. 

Wakristo kote duniani hii leo wanasherehekea Krismasi, kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

NIGERIA

Kiasi ya watu 100 wanaripotiwa kuuawa baada ya mlipuko kutokea katika kiwanda cha gesi nchini Nigeria. Mlipuko huo umetokea hapo jana kusini mashariki mwa Nigeria katika mji wa Nnewi. Ripoti zinaarifu kuwa mlipuko huo ulitokea wakati lori moja lilipokuwa likitolewa gesi ya kupikia. Idadi ya waliouawa katika mkasa huo hata hivyo inatofautiana huku polisi wa eneo hilo wakisema ni watu sita pekee waliokufa na wanahabari waliokuwa katika eneo la mkasa wakisema ni takriban watu 100. Waliofariki na majeruhi walipelekwa katika hospitali ya chuo kikuu cha Nnamdi Azikiwe. 

UTURUKI

Wanajeshi wa Uturuki wamewaua wanamgambo sita wa Kikurdi katika mapambano kusini mashariki mwa nchi hiyo na askari mmoja miongoni mwa watatu aliyejeruhiwa wakati wa mashambulizi hayo alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitalini. 

Tangu kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya wanamgambo wa chama cha wafanyakazi kilichopigwa marufuku nchini humo cha PKK na vikosi vya serikali ya nchi hiyo mwezi Julai mwaka huu, mgogoro umeibuka kwa mara nyingine katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo ambao tayari umesababisha vifo vya watu 40,000 hadi sasa. 

Mapigano hayo ya hivi karibuni yametokea hapo jana jioni katika mji wa Cizre ulioko karibu na mpaka wa Syria ambao umeghubikwa na mapigano makali tangu kuanza kutekelezwa kwa amri ya kutotoka nje siku kumi na mbili zilizopita, katika eneo hilo na katika mji ulioko karibu wa Silopi.

MALAWI

Malawi imewasimamisha kazi maafisa 63 wa umma wanaodaiwa kuiba mamilioni ya dola zilizotolewa na Marekani kama msaada wa kufadhili miradi ya kupambana na virusi vya HIV na ukimwi nchini humo.Waziri wa afya wa Malawi Peter Kumpalume amesema maafisa wa ngazi ya juu katika wizara hiyo wamesimamishwa kazi ili kuruhusu wahasibu kufanya uchunguzi wa jinsi fedha zilivyotumika katika wizara hiyo. Hiyo ndiyo idadi kubwa zaidi ya maafisa wa serikali kusimamishwa kazi katika taifa hilo la kusini mwa Afrika. Balozi wa Marekani nchini Malawi Virginia Palmer amesema anatumai maafisa wataweza kuwatambua waliohusika na wizi huo na kuchukuliwa hatua kali kwa kupora fedha zilizopaswa kusaidia kuboresha viwango vya afya vya raia wa Malawi. 

DRC

Kituo kimoja cha redio katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kimeripoti kuwa ndege moja ya mizigo ilipoteza mwelekeo katika uwanja wa ndege ulioko katika mji wa Mbuji Mayi na baadaye kupitiliza na kuingia katika eneo la makazi na kuua kiasi ya watu saba. 

Wakaazi wa eneo hilo wamekieleza kituo hicho cha Radio kuwa kulikuwa na hali mbaya ya hewa iliyolazimisha ndege hiyo kutua katika uwanja huo wa ndege kabla ya kupitiliza na kuingia katika makazi ya watu. 

Gavana wa eneo hilo Alphonce Ngoyi Kasanji amesema uchunguzi juu ya tukio hilo tayari umeanza. 

Taarifa za serikali zimearifu kuwa wafanyakazi wanne waliokuwemo ndani ya ndege hiyo hawakupata majeraha yoyote. 

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / KIMATAIFA KUTOKA DW SWAHILI KWA LEO DISEMBA 25/ 2O15

No comments :