Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » WANASINGIDA WAMETAKIWA KUTUMIA VEMA FURSA YA MATIBABU ZA MADAKTARI BINGWA MKOANI HUMO
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

SINGIDA.

Serikali mkoani  Singida, imewataka wananchi kuhakikisha wanatumia vyema fursa ya uwepo wa huduma zinazotolewa na madaktari bingwa, ili waweze kupatiwa ufumbuzi wa matatizo ya maradhi mbalimbali yakiwemo ya moyo na koo.

Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma zitakazotolewa kwa kipindi cha wiki nzima na madaktari bingwa katika  hospitali ya mkoa kwa kusema mpango wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) kuleta madaktari bingwa watano wa magonjwa mbalimbali mkoani hapa, utawapa nafasi wananchi wengi  kupata huduma na ushauri ambao hulazimika kuutafuta nje ya mkoa,hata kuvuka mipaka na kwenda nchi jirani.

Akifafanua zaidi, Dk.Kone amesema kwa miaka mingi  wakazi wa mkoa huu wamekuwa wakiingia gharama kubwa kusaka huduma za madaktari bingwa,hivyo uwepo wa madaktari hao hivi sasa,utawapunguzia gharama kwa wale watakaobahatika kuonana nao.

Aidha mkuu huyo wa mkoa ameupongeza kwa dhati uongozi wa NHIF, kwa kubuni mpango huo ambao una umuhimu na manufaa makubwa, kwa wakazi wa mkoa wa Singida.

Awali, Kaimu mkurugenzi mkuu NHIF, Michael Mhando,ameeleza lengo la mpango wa kupeleka madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali mikoani, ni kuwapunguzia wananchi adha ya upatikanaji wa madaktari bingwa mpango ambao unatoa huduma kwa wananchi bila kujali kipato chake, ambapo hadi sasa umefikia mikoa 13 ukiwemo mkoa wa Singida, zoezi ambalo ambalo litaendelea katika mikoa yote nchini.

Mbali kutoa huduma ya za kiafya pia wametoa msaada wa vifaa vya tiba na mashuka 300, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano, huku akiahidi mfuko huo kuendelea kuiunga mkono serikali ya mkoa kwa kuboresha sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Rufaa.

Wakati huo huo Mchungaji wa kanisa la kilokole la Pentekoste kijiji cha Itaja tarafa ya Mgori wilaya ya Singida David Mtipa (59) na mke wake Maria Philipo (45),wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa, kwa kosa la kushindwa kumpatia huduma muhimu mtoto wao, na kumsababishia madhara ya kudumu kiafya .

Wana ndoa hao wanatuhumiwa kushindwa kumpatia huduma muhimu mtoto wao Timotheo (30) kwa kipindi cha miaka 12 mfululizo.

Mapema mwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali,Patrisha Mkina,alidai mbele ya hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo,Faisal Kahamba,kuwa kati ya mwaka 2003 na 2015,kwa makusudi mchungaji David akishirikiana na mke wake Maria,walishindwa kumpatia mtoto wao Timotheo huduma muhimu za kibinadamu.

Aidha ameongeza kuwa wana ndoa hao walitenda kosa hilo,huku wakijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria namba 229 kanuni ya adhabu ujazo wa pili wa sheria kama ilivyofanyiwa marekebesho mwaka 2002.

Akifafanua,Mkina amesema kwa kipindi cha miaka 12,washitakiwa kwa pamoja walimnyima Timotheo,makazi,chakula,nguo,matibabu na uhuru wake wa kikatiba,kitendo ambacho kimechangia apate madhara ya kudumu ya afya yake.

Washitakiwa kila mmoja kwa wakati wake wamekana shitaka hilo,na kesi hiyo itatajwa tena desemba 28 mwaka huu.

Aidha,washitakiwa wapo rumande ya magereza baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni,kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini dhamana ya shilingi milioni moja kila mmoja.

Wakati huo huo,Joshua (25) mdogo wake na Timotheo,amesema baada ya wazazi wake kupelekwa rumande,ameshindwa kumpeleka kaka yake nyumbani licha ya kuruhusiwa kutoka wodi namba nne katika hospitali ya mkoa mjini hapa.

Mwandishi: Ramadhan Rajab
kutoka Singida
18/12/2015
mhariri: Denis Kazenzele

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / WANASINGIDA WAMETAKIWA KUTUMIA VEMA FURSA YA MATIBABU ZA MADAKTARI BINGWA MKOANI HUMO

No comments :