Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » » MAWAZIRI WA PUIGDEMONT WAWEKWA KOROKORONI, RAIA WA CATALONIA WAANDAMANA BUNGENI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Raia wa jimbo la Catalonia wanaotaka kujitenga wameandamana nje jengo la bunge la jimbo hilo mjini Barcelona baada ya jaji mjini Madrid kuwaweka kizuizini mawaziri nane wa serikali ya jimbo la Catalonia.

Taarifa zinasema kuwa hadi sasa kuna jumla ya wanasiasa kumi wa Catalonia waliowekwa kizuizini nchini Hispania wakiwemo pia viongozi wa kitamaduni wawili ambao nao wanashikiliwa.

Waandamanaji hao wamesikika wakiimba kuwa Hispania ni aibu ya Ulaya.

Jaji Carmen Lamela amesema kuwa aliamua kuwaweka kizuizini viongozi hao nane kwa kuhofia kwamba wanaweza kutorokea nje ya nchini ama kuharibu ushahidi.

Waendesha mashitaka wanawatuhumu wanasiasa hao kwa makosa mawili ambayo ni mapinduzi na uchochezi katika jaribio la kutaka kujitenga na Hispania.

Hata hivyo jaji bado hajatoa kibali cha kukamatwa nje y nchi kwa kiongozi wa watu wa jimbo la Catalonia Carles Puigdemont na wenzake wane ambao wote wapo nchini Ubelgiji.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / / MAWAZIRI WA PUIGDEMONT WAWEKWA KOROKORONI, RAIA WA CATALONIA WAANDAMANA BUNGENI

No comments :