WAENDESHA Bodaboda 400
wa manispaa Dodoma wameanza kunufaika na ahadi za Mbunge wa jimbo hilo Anthon
Mavunde kwa kuanza kupatiwa mikopo ya Pikipiki za mataili matatu na mawili kwa
bei nafuu ili kukuza na kuendeleza mitaji yao ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Akiongea katika
mahojiano na kipindi cha Dodoma 24 kinachorushwa na kituo cha Redio cha Rasi Fm
cha mjini humo Mshauri wa kampuni ya kutoa mkopo nafuu [TLF] Godbless George
ambapo amesema kampuni hiyo imeingia
mkataba na Mbunge wa jimbo hilo kwa ajili ya kuwawezesha vijana kama
utekelezaji wa Ahadi zake
Amesema kwa awamu ya kwanza wameanza na vijana 400 wanaopitia katika chama cha waendesha
Bodaboda Wilaya ya Dodoma Mjini ambapo
kwa sasa wameanza kuwapa mafunzo ya namna ya kuzitumia pikipiki hizo ambazo
malengo yake ni kuwainua kuiuchumi.
Aidha Mshauri huyo
amesema vijani hao kama wataweza kuzingatia misingi ya uendeshaji huo na kuwa
na nidhamu katika mapato yake na dhahili kuwa watapiga hatua za kimaendeleo
ambapo kila mmoja anatakiwa kufanya marejesho ya 7000 kwa siku tofauti na
kampuni nyingine zinazotoza Elfu kumi kwa siku.
Huyu hapa ni Mshauri wa kampuni ya kutoa mikopo nafuu [TLF] Godbless George akitoa ufafanuzi kwa ufupi juu ya zoezi hilo
No comments
Post a Comment