Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MAJIPU MENGINE YAPO KWENYE ARDHI VIJIJINI KAMA HILI LA MWANAKIJI MWENYE FEDHA KUWANYANYASA WANAKIJIJI KISA FEDHA ZAKE...{HABARI & PICHAZ}
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Joyce Fundi miaka 982) mwenye Jembe akieleza jambo kuhusu Makaburi hayo na Jinsi shamba lake pamoja na ya wakulima wengine yalihatalini kutaifishwa. IMETENGENEZWA NA BANDA BLOG

Moja ya Kaburi lililopo katika Mashamba hayo yenye Mgogoro katika ya wakazi wa Mapinduzi na Mwenzao kijini hapo, Kaburi hilo lilizikwa mwak 1958

Baadhi ya wakulima wa Kijiji cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika katika Eneo la Mgogoro ambalo walikuwa wakilitumia kwa kilimo.

Na John Banda, Dodoma

ZAIDI ya Wakulima 60 wa Kijiji cha Mapinduzi ‘A’ kata ya Nghong’onha  manispaa ya Dodoma wanawasiwasi wa kunyang’anywa mashamba yao yenye ukubwa wa Hekari 237 kutokana na mkazi mwenzao aliye na nia ya kuwadhulumu kwa vitisho vya kutumia polisi ikiwemo kuburuzwa mahakamani huku wakikosa msaada wowote toka kwa viongozi wa ngazi za juu.

Wakizungumza na waandishi wa habari Kijijini hapo wakulima hao walisema wamekuwa wakipata wakati mgumu tangu mwaka 2012 ambapo Bwana Mchiwa Chedego alipowaomba wamuuzie mashamba ili ayatumie kwa kilimo cha zabibu wakamkatalia na ndipo akaanza visa vya kuwakamata na kuwapeleka kwenye mabaraza ya ardhi ngazi za kijiji na kata ambako walishinda na baadae akawahamishia Wilayani.

Kwa upande wake George Chidawili (91) alisema walipopelekwa baraza hilo la Ardhi la Wilaya walishangaa wameongezeka mpaka kufikia 11 na baadae kuongezeka na kufikia 17 na hivi karibuni akakamatwa na mwenyekiti wa Kijiji hicho Willy Joseph na kufikia watu 18 waliofikishwa mahakamani ambapo hali hiyo imekuwa ikiwafanya kushindwa kufanya shuhuli zao za kimaendeo badara yake wana wamekuwa wakihudhuria keshi hizo mahakamani na polisi.

Alisema kati ya mwaka 2012/15 tayari Chedego alishawapeleka wazungu wawili katika eneo hilo kwa nia ya kuwaonyesha kama panafaa kwa kilimo cha zabibu hali ambayo inaashiria kuwa tayari mashamba yao yameshauzwa kwa wazungu hao.

“Wajukuu zangu tumepata shida sana mpaka kufikia sasa maana tunaona kama vile serikali nzima kaiweka mfukoni mwake, hivi kweli mtoto aliyezaliwa tunamuona kupata hivyo vihela anataka kutukalia vichwani na hivi huwa tunapata taabu sana kwa sababu wakati mwingine hujifanya kama siyo Mgogo maana hata huko polisi na mahakamani mwenzetu anaongeaga kizungu hata Kiswahili hataki hali inayowafanya hata baadhi ya polisi kumuogopa,
Na hao wazungu anaokujaga nao na kwenda kuwaonyesha  mashamba yetu kwa sasa hatutakubali watakapokuja tutawafukuza hatatakubali kuona mashamba ambayo tunayategemea kwa chakula cha familia zetu mtu mmoja aje kutunyang’anya na kuyauza kwa ajili ya tama zake”, alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Hicho Willy Joseph alisema Tayari kijijini hapo kuna viashiria vya uvunjifu wa amani kutokana na wakazi wengi kutopendezwa na kitendi hicho cha ndugu zao kutishiwa Maisha na mara nyingi kukamatwa na kufikishwa polisi na mahakamani kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kuvamia shamba lake, kumtishia na mengineyo huku akiwachonganisha na polisi kuwa wakazi hao wanaongoza kwa fujo huku wakiwakataa kufika kijijini hapo.

Aliongeza kuwa  hata yeye anashangazwa na kitendo cha kukamatwa kwake akidaiwa kuongoza fujo kijijini hapo, ambapo aliitaka serikali kupitia vyombo vyake kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mgogoro huo ambao ulianza kufukuta miaka 4 iliyopita ili kuwasaidia wakazi hao waweze kuishi na kulima kwa amani katika katika mashamba waliachiwa na Mababu na Bibi zao.

Nae Diwani wa Kata ya Nghon’oha Philip Namga alisema kuwa Mgogoro huo ameukuta ni wa Muda mrefu sasa lakini hawezi kuuzungumzia kwa kuwa shauri hilo lipo mahakama ya Wilaya lakini kwa sasa anamsubiri Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthon Mavunde ambaye kwa sasa Yupo jijini Dar es Laam kwa shuhuri za kiserikali ili afikishie Taarifa hiyo ili ajue jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wake.

Hata hivyo Gazeti hili lilishuhudia uhalibifu mkubwa wa kukatwa kwa mazao mbalimbali yakiwemo mahindi, Alizeti na mtama yakiwa yamefyekwa katika moja ya shamba kijijini hapo na watu wasiyojulikana, ambapo wadadisi wa mambo wanasema kuwa inawezekana kuwa ni ulipaji  kisasi kutokana na hilo kuwa tukio la tatu katika mashamba tofauti.

Bado juhudi za kumapata Chedego ili aweze kutoa ufafanuazi wa Tuhuma dhidi yake zinaendelea kutokana na kutokuwepo kijijini hapo wakati waandishi walipofanya ziara kijijini hapo.

Picha: na John Banda
mhariri:Denis J Kazenzele
feb/18/2016 Alhamis

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MAJIPU MENGINE YAPO KWENYE ARDHI VIJIJINI KAMA HILI LA MWANAKIJI MWENYE FEDHA KUWANYANYASA WANAKIJIJI KISA FEDHA ZAKE...{HABARI & PICHAZ}

No comments :