Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » DIWANI WA CCM ATUHUMIWA KUKACHA UZINDUZI WA KIKUNDI CHA WALEMAVU.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na Peter Mkwavila,Dodoma.
CHAMA cha watu wenye ulemavu wasioona wilaya ya Dodoma kimemtuhumu diwani wa kata ya Mnadani Farida Mbaruku (CCM) kwa kile walichodai kuingia mitini kwa kutoonekana kwenye uzinduzi wa mradi wa uuzaji wa vinywaji baridi wa kikundi cha Imani cha akina mama wasiona 
Wakizungumza kwa huzuni na masikitiko akina mama hao ambao walio wengi wana ulemavu wa kutoona,wamesema kuwa kitendo hicho kinaonyesha ni jinsi gani ambavyo wao wanajiona wana nyanyapaliwa na kiongozi wao waliyemchagua kwa lengo la kushirikiana katika shughuli za kimaendeleo.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Magrent Mwaluko amesema kuwa lengo la kumshirikisha katika tukio hilo ni kuwazindulia mradi huo ambao wameamua kuungana kwa pamoja na kuanzisha ili waweza kuondokana na tabia ya kwenda mitaani kuombaomba kwa wasamaria wema na hatimae.waweze kujitegemea wenyewe.

“Lakini kwa kweli diwani wetu ametusikitisha kwa kutofika kutuzindulia mradi huo pamoja na kumpelekea barua ya mwaliko kama mgeni rasm hajatokea hii inaonekana kutunyanyapaa kwa hata taarifa hatukupatiwa kama hatoshiriki na sisi kwenye uzinduzi huo”alisema.

Mwaluko amesema kuwa kuwepo kwake pia kungesaidia kuchangia na kuwaunganisha kwenye taasisi zinazokopesha fedha ili waweze kuwezeshwa kwa lengo la kuukuza mradi huo na hatimaye waweze kukokopeshana wenyewe na kuweza kumudu maisha yao.

Naye Mwenyekiti wa chama cha wasiona wilaya ya Dodoma Iddy Abdalah akizungumza na akina mama wa kikundi hicho pamoja na viongozi wa vyama vya mbalimbali vya ulemavu vilivyohudhiria kwenye uzinduzi huo wa kikundi amesema kuwa kitendo cha kutoshiriki diwani huyo akijafurahiwa na wanaamini kiongozi huyo kama angealikwa na Rais,mkuu wa mkoa au wa wilaya,ni imani yao asingeingia mitini lakini kwa kuwa ni wao walemavu ndiyo maana wametendewa hivyo..

Amesema yeye kama kiongozi alistahili kutoa taarifa mapema kama hatoshiriki na badala yake angetakiwa kumtuma mwakilishi wake ili aweze kuwakilisha na hatimaye wakashiriki katika zoezi hilo muhimu ambalo lilikuwa la kujikomboa kiuchumi kwa akina mama hao.

Akijibu tuhuma hizo Diwani wa kata hiyo ya Mnadani kwa tiketi ya chama cha mapinduzi {CCM}Farida Mbaruku  kwa njia ya simu amesema kuwa ameshindwa kushiriki kutokana na kuwa nje ya mkoa wa Dodoma na siyo kweli kama anavyotuhumiwa kuwa amewanyanyapaa wanawake hao.

“Ni kweli nilipatiwa barua ya mwaliko lakini nilitegemea kuwahi lakini nimechelewa kufika kwenye uzinduzi huo, na hapa tunapoongea na wewe nipo kwenye gari ninatoka Dar-es-Salaam ambako nilimpeleka mtoto wangu kutibiwa na kama sivyo hivyo ningeweza kushiriki katika uzinduzi huo ambao mimi mwenyewe nilikubali kuwa mgeni rasim”amesema..

Ameongeza kuwa kuwepo kwa kikundi hicho cha akina mama wasioona ndani ya kata hiyo ni jambo jema kwani kitawasaidia kupata mikopo kwa kupitia mradi huo ambao wameuanzisha kwa malengo ya kujikomboa kiuchumi na kuondokana na tabia ya kuombaomba mitaani.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / DIWANI WA CCM ATUHUMIWA KUKACHA UZINDUZI WA KIKUNDI CHA WALEMAVU.

No comments :