Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » » HII NAOMBA IKUGUSE: MLEMAVU AOMBA AJIRA KWA WATANZANIA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Hujafa hujaumbika! Erasto Mketo (26) ni mkazi wa Lindi kijiji cha Mtondo Kimwaga, ni
mlemavu wa miguu na mikono ambaye ana ndoto nyingi za kujikwamua kimaisha kama
kijana mwingine wa Kitanzania, lakini ulemavu wake umekuwa changamoto kubwa ya
yeye kuweza kufanikisha ndoto zake.

Moja ya changamoto zinazomkuta Erasto ni pamoja na unyanyapaa hasa kwenye sekta ya
ajira jambo lililomfanya apaze sauti na kuwaomba Watanzania wajitokeze kumsaidia hata kwa kumpa mtaji au ajira ili aweze kujikwamua kimaisha.

Akiongea na mwandishi wa Blogs za Mikoa Tanzania, Erasto alisema anaamini anaweza kufanya biashara yoyote kama muajiriwa au kama atapewa mtaji wa kufungua biashara yake mwenyewe.

“Kwa huku kijijini nimekuwa nikipata tabu sana ya kupata ajira ambayo itaendana na ulemavu wangu na elimu yangu ya shule ya msingi, lakini ningependa sana nitimize ndoto zangu kwa sababu naweza sana kufanya biashara.

“Nawaomba watanzania wenzangu mnisaidie hata kwa kuniajiri ili mradi na mimi nijikwamue
kiuchumi kama wenzangu na hata niweze kuwasaidia wazazi wangu,” alisema Erasto huku akiongeza kuwa baiskeli ya kutembelea atainunua mwenyewe kupitia ajira yake ikiwa atapata mtu wa kumuajiri.

Kutoa ni moyo si utajiri, kama umeguswa tafadhali msaidie Mtanzania mwenzako kwa hali na mali  kupitia namba 0682755874, imesajiliwa kwa jina la Anastansi Ngomba.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / / HII NAOMBA IKUGUSE: MLEMAVU AOMBA AJIRA KWA WATANZANIA

No comments :