Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

Ayman Safadi alisema alimuambia waziri wa mashauri wa nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson kuwa hatua kama hiyo inaweza kuzua ghadhabu kubwa kwa nchi za kiarabu na ulimwengu wa kiisalmu.

Kuna uvumi kuwa Rais Donald Trump atatangaza hilo hivi karibuni na kutimiza ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni.

Jared Kushner, mkwe wa Trump alisema kuwa bado hakuna uamuzi uliofanywa.

Katika mtandao wa Twitter, Bw Safadi alisema: #Nilizungumza na waziri Rex Tillerson kuhusu hatari ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. 

Hatua kama hiyo inaweza kusababisha ghadhabu kwenye nchi za kiarabu na kwa ulimwengi wa kiislamu na kuzua misukosuko na pia kuhujumu jitihada za amani."
 
Hakuna jibu lolote kutoka kwa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani.
Naye rais wa Palestina Mahmoud Abbas anajaribu kupata uungwaji mkono wa kimataifa katika kumshawishi Trump asifanye tangazo kama hilo.

Ofisi yake ilisema kwa aliwapigia simu Jumapili viongozi wa dunia wakiwemo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

"Alitaka kulezea harari za uamuzi wowote wa kuhamisha ubalozo wa Marekani kwenda Jerusalem au kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Isael," mshauri wa Bw. Abbas, Majdi al-Khalidi aliliambia shirika la AFP.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Jardan ameonya Marekani kuhusu hatari ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Wakati picha za majengo yenye nyufa zikisambaa mitandaoni ikidaiwa ni ya hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umekwenda kukagua ili kujiridhisha.

Majengo hayo yaliyojengwa na TBA kwa miezi minane yakielezwa kugharimu Sh10 bilioni yalizinduliwa Aprili 15,2017.

Ujenzi ulifanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kumaliza tatizo la malazi kwa wanafunzi wa UDSM.

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga, jana alisema hata yeye ameziona picha hizo kwenye mitandao ya kijamii.

“Nimeziona na muda huu najiandaa kwenda huko kuangalia kama taarifa hizo ni za kweli,” al;isema Mwakalinga 

Picha hizo zilianza kusambaa jana jioni. Mwakalinga alisema huenda picha hizo ni za majengo mengine lakini zimehusishwa na hosteli hizo.

“Nitatoa taarifa baada ya kukagua majengo hayo kwa sasa siwezi kuzungumza hadi nitakapoona,” alisema.

Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji amepita katika mchakato wa kumtafuta muwekezaji wa klabu ya Simba na ofa yake ya Tsh bilioni 20.

Dewji ambaye amejitokeza na kuwa muwekezaji pekee ambaye aliweka dau kubwa la Tsh bilioni 20 kupata hisa kwa asilimia 51 ndani ya klabu hiyo amekubaliwa kwa dau hilo kwa kupata hisa 49.

Mwenyekiti wa kamati ya mchakato huo wa mabadiliko, Jaji Mihayo amesema, Mo Dewji amepita na kitachofuatia ni majadiliano mengine baada ya mkutano wa jana.

“Mohammed Dewji ndiye mshindi, maana katika kamati yetu. Hivyo yeye ndiye amekuwa mshindi wa kuwania kuwekeza katika klabu ya Simba. Baada ya mkutano huu kutakuwa na majadiliano,” amesema Jaji Mihayo.

Hata hivyo Mwekezaji huyo mpya katika klabu ya Simba, amesema amejipanga kushirikiana na wanahisa wenzake wa klabu hiyo kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kupitia kampuni ya Simba Sports Club Limited.

Dewji ameyasema hayo wakati akitoa salamu kwa wanachama na mashabiki wa Simba kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo, baada ya kutangazwa na kamati maalum ya kusimamia mchakato wa kumpata mwekezaji katika klabu ya Simba, kuwa mshindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu hiyo.

Amesema klabu ya Simba inampongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuongoza serikali ya awamu ya tano, na wao wamedhamiria kuhakikisha wanakwenda sambamba na kasi yake kupitia mchezo wa mpira kwa kutoa ajira kwa Watanzania kwenye kampuni mpya itakayosimamia timu hiyo katika mfumo wa hisa.

“Tamati yangu nielekeze kwa sisi sote kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayofanya ya kuongoza taifa hili. Wote tumtakie kila la kheri, baraka na fanaka tele katika utumishi wake uliotukuka,
“Pamoja na kupongeza sera yake ya ujenzi wa viwanda nchini, ambapo sisi kwa upande wetu, klabu ya Simba inamuunga mkono kwa ujenzi wa kiwanda kikubwa kabisa cha soka yaani Simba Sports Club Limited, ambacho licha ya kuongeza ajira lakini pia tutaendelea kulipa kodi kwa mujibu wa sheria za nchi,” alisema Dewji.

Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohammed Entreprises, ametumia mkutano huo kuelezea mipango ambayo wameipanga ili kuiwezesha Simba kuwa klabu kubwa zaidi barani Afrika kuliko ilivyo sasa, huku malengo ikiwa ni kuwania mataji makubwa barani Afrika.

“Katika mwaka wa kwanza, nawaahidi kwa kushirikiana na ninyi tutakuwa na kiwanja cha nyasi asilia, na kiwanja cha nyasi za bandia ambapo viwanja hivi tutavitumia kwa mazoezi kwa kadri ya mahitaji ya mechi tunayokwenda kucheza,.

“Pia tutajenga hosteli ambayo itakuwa na vyumba 35 ambavyo wataishi wachezaji 30 na support staff, kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 35 square- meter… ili kufanya eneo hilo kuwa bora kwa wachezaji wetu,” alisema Dewji na kuongeza.

“Wote tunaopenda mpira, tunajua kama ukitaka kuwa na wachezaji bora lazima utumie pesa. Nia yetu kwa mwaka wa kwanza, tunatarajia kiwango cha chini cha pesa ya usajili iwe bilioni moja. Pia tumetenga milioni 500 kuboresha benchi la ufundi, kwa kushirikiana na benchi liliopo sasa.”

Hata hivyo Dewji, alisema klabu ya Simba itajenga kituo cha kukuzia vipaji ambacho kitakuwa na wachezaji vijana. Jambo ambalo litaisaidia Simba kuwa na wachezaji bora vijana ambao wamefundishwa kucheza soka katika kituo cha timu hiyo.

“Ili kuwa na wachezaji bora kwa miaka ijayo tunahitaji kuwa na kituo cha kukuzia vipaji kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 14, 16, 18. Na mipango yetu ya baadae ni kushirikiana na timu kubwa za ulaya kutuongoza na kutuelemsha jinsi gani ya kujenga kituo chenye hadhi ya kimataifa na mungu akipenda tutakuwa na kituo bora barani Afrika.” alisema Dewji.

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah akimkabidhi cheti cha ushindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu ya Simba mfanyabiashara na mwanachama wa muda mrefu wa klabu hiyo, Mohammed Dewji MO kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekanusha habari inayoenea kuhusu Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kujivua uanachama kuwa hazina ukweli wowote na zinapaswa kupuuzwa.

Chadema wametua kanusho hilo kupitia mtandao wa Twittter kwenye ukurasa wa chama hicho na kusema kwamba wanaosambaza habari za Mnyika kujivua ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya maisha ya watanzania.

"Kuna taarifa zinasambazwa mitandaoni ya kuwa Mhe. John Mnyika, Mbunge wa Kibamba amejivua uanachama wa CHADEMA. Taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote, ni za kupuuzwa, wanaozisambaza ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya hali ya maisha ya Watanzania".

Korea Kaskazini imesema Rais Donald Trump wa Marekani na serikali yake "wanabembeleza vitokee vita vya nyuklia" huku Washington na muitifaki wake katika Peninsula ya Korea, yaani Korea Kusini zikijiandaa kufanya manuva makubwa ya kijeshi ya angani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imeeleza katika taarifa iliyotoa hapo jana kuwa Trump anaanzisha mchezo hatari wa kamari ya nyuklia katika Peninsula ya Korea na kumwita rais huyo wa Marekani 'jini mbaya wa nyuklia' na 'mvurugaji amani ya dunia'.

Taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini imetolewa katika hali ambayo Marekani na Korea Kusini zinajiandaa kwa mazoezi ya kijeshi yaliyopewa jina la Vigilant Ace yaliyopangwa kuanza Jumatatu ya kesho. Askari wapatao 12,000 wa jeshi la Marekani na ndege za kivita 230 wanatazamiwa kushiriki kwenye manuva hayo.

Hayo yanajiri huku kauli za vitisho zinazotolewa na Marekani dhidi ya Korea Kaskazini zikikabiliwa na ukosoaji mkali.

Baada ya Korea Kaskazini kulifanyia majaribio kombora lake la balistiki la masafa marefu zaidi, mapema wiki hii balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley aliionya serikali ya Pyongyang kuwa nchi hiyo inaweza "kuangamizwa kikamilifu" endapo vita vitatokea kati yake na Washington.

Hata hivyo matamshi hayo ya Haley yalikosolewa vikali na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov, ambaye siku ya Ijumaa alisema: "kama kuna mtu aliyedhamiria kikweli kutumia nguvu, kama alivyoeleza mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ili kuiangamiza Korea Kaskazini.. nadhani atakuwa anachezea moto na kufanya kosa kubwa".

Korea Kaskazini inakabiliwa na vikwazo mbalimbali vya kimataifa vya kuishinikiza isimamishe mipango yake ya nyuklia na makombora. Hata hivyo imepuuza mashinikizo yote yanayotolewa dhidi yake huku ikiapa kuwa haitoachana na mipango yake ya nyuklia na makombora kutokana na vitisho na uadui wa Marekani dhidi ya nchi hiyo.

Latest Post