SHIRIKA la Umeme Tanzania(TANESCO) mkoani Kagera limesema liko tayari kulipa fidia kwa mteja yeyote atayepata madhara yanayosababishwa na kukatika-katika kwa umeme,iwapo itathibitika kuwa chanzo cha hitilafu ni shirika lenyewe.
Kauli hiyo kutoka shirika hilo mkoani humo imetolewa baada ya
wateja wengi kulalamikia shirika hilo,kwa kile kinachodaiwa kukata umeme
bila kuwataarifu na kuwasha umeme ghafla,hali inayosababisha wateja
wengi kuunguza mali zao,ikiwa ni redio,Luninga,firiji n.k.
Akitoa ufafanuzi juu ya kero hiyo kubwa kwa wateja wengi hasa
wadogo na wakubwa mkoani hapa,Mhandisi Mwandamizi kitengo cha Usambazaji
wa shirika hilo mkoani hapa Felix Olan’g,amesema kuwa changamoto hiyo
inatokana na ya wateja wengi kuongeza kwa matumizi ya umeme kwa kuongeza
vifaa vingine vinavyotumia umeme tofauti na maelezo yao ya
awali,ambavyo kila mteja ulazimika kuwa wazi wakati akiomba huduma ya
umeme.
Hata hivyo,Olan’g amesema kuwa Tanesco iko tayari kumlipa mteja
yeyote anayeweza kudai fidia halali,ikiwa atapata madhara
yatakayothibika kusababishwa na shirika hilo,ilimradi madai ya vifaa
vitakavyodaiwa kuungua viendane na maelezo ya awali yaliyotolewa wakati
wa maombi ya huduma ya umeme.
Ameongeza kuwa mteja anapaswa kutoa taarifa kwa ya matumizi ya
umeme wake hasa pale anapoongeza hitaji kwa kuongeza vifaa vingine
katika nyumba yake kwani huduma inayotolewa na shirika inategemeana na
matumizi ya mteja.
Hapo awali katika swali lililoelekezwa kwa Tanesco mkoa wa Kagera
na Afisa Mwandamizi Idara ya Mafao kutoka shirika la hifadhi ya
jamii(NSSF) mkoa wa Kagera Gerad Mkonyi,wakati kikao cha watendaji wa
Tanesco na wateja wakubwa wa Umeme mkoani hapa,alitaka kujua kama
shirika hilo(Tanesco)lina utaratibu wa kuwalipa wateja waliounguliwa
vifaa vyao kutokana na tabia ya shirika la Tanesco kukata umeme na
kuwasha bila taarifa kwa wateja.
Akijibu swali hilo Kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Kagera Mhandisi
David Mhando,amesema kuwa Tanesco haitahusika kamwe kulipa wateja
wataounguliwa vifaa vyao kutokana na sababu itayobainika kusababishwa na
mteja mwenyewe au wateja wengine.
Kikao cha Tanesco na wateja wakubwa wenye viwanda mkoani hapa
kiliandaliwa kwa madhumuni kupata changamoto na kutafuta jinsi ya
kuzitatua,huku kati ya wateja shirika hilo mkoani hapa ni 51,042 wateja
42 tu ni wateja wakubwa wa viwanda.
Kwa mujibu wa Mhasibu wa Tanesco mkoani hapa Leonard Mayunga wateja
hao 42 wanachangia asilimia 41%ya pato la mkoa huku wateja wadogo na wa
kati uchangia asilimia 59% tu.
No comments
Post a Comment