Wafungwa 6 wa kike wanaoshikiliwa katika jela ya mji wa New York
nchini Marekani wamewasilisha mashtaka ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia
na maafisa wa jela hiyo.
Wahanga hao wa unyanyasaji wa kingono katika jela ya New York
wamewasilisha mashtaka yao katika Mahakama ya Federali ya Manhattan
wakisema kuwa maafisa wa jela hiyo wamekuwa wakifumbia jicho unyanyasaji
wa kingono wanaofanyika katika jela hiyo. Wamesema kuwa kila mara wanapowasilisha mashtaka na kufanyiwa ukatili wa kingono wamekuwa wakikabiliwa na mashinikizo makubwa zaidi.
Wiki iliyopita pia afisa wa polisi ya jimbo la Oklahoma nchini Marekani alihukumiwa kifungo cha miaka 263 ambacho ndicho kifungo cha juu zaidi nchini humo baada ya kupatikana na hatia ya kubaka wanawake kadhaa akiwa kazini.
Ripoti ya kila mwaka ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International pia imelalamikia ukiukwaki wa haki za binadamu unaofanyika nchini Marekani kama mateso yanayofanywa na maafisa wa shirika la ujasusi la nchi hiyo CIA dhidi ya mahabusu waliokamatwa kinyume cha sheria na utumiaji wa mabavu wa polisi ya nchi hiyo.
No comments
Post a Comment