Naibu Waziri wa Afya, Dk.
Kigwangalla akitoa hutuba fupi wakati wa tukio hilo la kambi maalum ya
matibabu ya bure kwa wananchi wote iliyoandaliwa na Care Foundation kwa
kushirikiana na wadau wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Ilala, Mh.
Mussa Hazan Zungu.
………………………………………………………………………………………………………………………………….
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla amehimiza Jamii kuwa na utaratibu wa kupima afya mara
kwa mara katika hali ya kubaini matatizo yanayowakabili ilikuchukua
hatua ikiwemo kupata tiba mapema
Dk.
Kigwangalla ametoa kauli hiyo mapema leo Februari 28.2016, jijini Dar
es Salaam, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kambi maalum ya kupima
afya bure kwa wananchi mbalimbali wakiwemo wa Jimbo la Ilala kwa
kuandaliwa na Care Foundation na wadau wengine wa afya ikiwemo Hospitali
ya Ebrahim Haji Chartable Health Centre ambao wanasimamia kutoa huduma
za matibabu kwa kushirikiana na taasisi zingine.
Akitoa
hutuba yake fupi, kwa wananchi mbalimbali walifika katika tukio hilo la
kupatiwa matibabu hayo ya bure, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla amesema
Jamii wanatakiwa kuwa na maisha yenye afya hivyo zoezi la kupima afya
mara kwa mara ni bora zaidi kaika kuimalisha afya ya mwili.
“Wananchi
wapo na wakati mwingi wakifanya shughuli zingine na hata muda kupima
afya inakuwa ngumu. Kukinga ni bora Zaidi kuliko tiba. Zoezi hili
litasaidia sana wananchi wengi na tunaomba muendelee na maeneo yote ya
nchi yetu.” Ameeleza Dk.Kigwangalla.
Aidha,
Dk. Kigwangalla amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Hazan Zungu
kwa kuwezesha kuandaa zoezi hilo kwa kushirikiana na wadau hao kwani ni
mfano bora wa kuigwa na wabunge wengine pindi wapatapo nafasi ya
kutumikia jamii iliyowachagua.
Pia
katika zoezi hilo, Mbune wa jimbo la Ilala, Mh. Mussa Zungu na Naibu
Waziri Dk. Kigwangalla walipata wasaha wa kupima afya zao pamoja na
kutembelea maeneo ya kutolea huduma na kushuhudia namna huduma
zinavyotolewa kwa wananchi.
Kambi
hiyo ya matibabu, inatoa matibabu hayo bure kwa wananchi wote wanaofika
hapo ambapo pia mbali na matibabu wanatoa huduma ya dawa huku wakitoa
pia mawani kwa watu wenye matatizo ya macho. Watu mbalimbali
wamekaribishwa kupatiwa matibabu hayo ambayo pia yanatolewa na madaktari
bingwa wa magonjwa husika.
Tukio likiendelea |
Naibu Waziri wa Afya. Dk.Kigwangalla akiwa katika vipumo hivyo.. |
Mbunge wa Ilala, Mh. Mussa Hazani Zungu, akipima afya katika zoezi hilo.. |
Dk. Efrahim Mika Zaky wa masuala ya macho, akimpima macho Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla wakati wa zoezi hilo.. |
Naibu Waziri Dk.Kigwangalla akiwa katika moja ya sehemu ya kutolea dawa na miwani kwa watu watakaobainika kuwa na matatizo katika macho.. |
Uchunguzi wa macho ukiendelea.. |
via fullshangwe.blogspot.com
No comments
Post a Comment