Jumapili ya February 28 Ligi Kuu Ubelgiji iliendelea tena kwa klabu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta kushuka katika uwanja wake wa nyumbani Cristal Arena kucheza mchezo wake wa 28 wa Ligi Kuu dhidi ya vinara wa Ligi Club Brugge.
Licha ya kuwa Club Brugge walikuwa wanarekodi nzuri dhidi ya Genk wamekubali kipigo cha goli 3-2, kwani kabla ya mchezo huo, Genk na Brugge kwa mechi tano zilizopita, Brugge walikuwa wameifunga Genk mara tatu, sare moja na kupoteza mechi moja.
Magoli ya KRC Genk yalifungwa na Nikolaos Karelis dakika ya 31, ikiwa ni dakika 21 zimepita toka Club Brugge wapate goli la kuongoza dakika ya 15 kupitia kwa Thomas Meunier, lakini kasi ya Genk iliongezeka na kupata goli la pili dakika ya 50 kupitia kwa Thomas Buffel.
Mbwana Samatta aliingia dakika ya 79 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis aliyefunga goli la kwanza la KRC Genk. mabadiliko ya kuingia Mbwana Samatta yalikuwa na faida kwani, dakika 2 baada ya kuingia alipachika goli lake la kwanza akiwa na Genk lakini pia ni goli la tatu kwa Genk, kabla ya dakika ya 83 Brugge walifanikiwa kupata goli la pili.
No comments
Post a Comment