Jumapili ya February 28 Kombe la FA Tanzania liliendelea kwa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa 16 bora dhidi ya klabu ya Singida United katika dimba la Taifa Dar Es Salaam.
Simba ambao waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupata majeraha ya kufungwa na Yanga katika mechi zao mbili za Ligi Kuu, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-1, hivyo Simba wametinga hatua ya 8 bora ya Kombe hilo.
Je baada ya hapo anakutana na nani? tusubiri kujua...
No comments
Post a Comment