Waziri mkuu Kassim Majaliwa |
Akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo leo (Jumapili, Februari 28, 2016), Waziri Mkuu alisema maafa huwa yanakuja bila kutarajiwa na akatumia fursa hiyo kuwashukuru wadau waliotoa misaada ya chakula, magodoro, mashuka, vitenge, mabati na mbegu za mazao.
Aliwataja wadau hao kuwa ni benki ya NMB, NSSF, wakazi wa Ruangwa na marafiki wa Ruangwa waishio Dar es Salaam ambao walifika kukabidhi misaada hiyo.
Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku mbili katika mikoa ya Mtwara na Lindi kukagua athari za mafuriko, hatua zinzochukuliwa za utoaji misaada kwa waathirika na kuwapa pole wananchi walioathirika na mafuriko hayo, alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi waishio mabondeni wahame kwa sababu mvua kubwa bado zinakuja.
“Jambo hili si mipango ya mtu
binafsi na sote tunajua kwamba tunahitaji mvua kwa ajili ya mazao lakini
safari hii zimekuja zaidi ya kiwango cha kawaida. Mamlaka ya hali ya
hewa imeshasema kuwa mvua kubwa zaidi zinakuja ifikapo Machi mwaka huu”,
alisema.
Ili kuepusha maafa zaidi, kuanzia
sasa, wale waliojenga mabondeni wanapaswa wahame. Pia nawasihi wananchi
wachukue tahadhari wakiona mvua inakuja na upepo mkali wasikae ndani ya
nyumba sababu hapa kijijini tumempoteza mzee wetu mmoja ambaye
aliangukiwa na nyumba baada ya nyumba yake kuangukiwa na mti kutokana na
mvua hizo,” aliongeza.
Kwa mujibu taarifa ya maafa
iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Bi. Mariam Mtima, mvua
zilizonyesha kati ya Januari na Februari mwaka huu zilisababisha nyumba
393 kuezuliwa na nyingine kubomoka na kuacha wakazi wa vijiji hivyo bila
makazi.
“Zahanati ya kijiji cha Mtondo
iliezuliwa paa, daraja la mto Muhuru limebomoka na halipitiki kabisa na
ekari 1,186 za mashamba ya wananchi zimesombwa na maji.
Mazao
yaliyoathirika ni mahindi, muhogo, mikorosho, mtama, ufuta, kunde,
mpunga na mbaazi,” alisema Mkuu huyo wa wilaya katika taarifa yake.
Alivitaja vijiji vingine ambavyo
mafuriko hayo yaliharibu mashamba ya wananchi kuwa ni Nambilanje,
Mkaranga, Namkatila, Chinongwe A, Likwachu, Nauname na Mbekenyera.
Alisema hali hiyo imesababisha
upungufu mkubwa wa chakula wilayani humo na sasa hivi wanahitaji tani
1,133 za chakula aina wanga ambazo anataraji zitatosheleza mahitaji kwa
mwezi Machi 2016.
No comments
Post a Comment