******************************
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechapuzwa kuendelea kuongeza nguvu zaidi katika uimarishaji wa Miundombinu ili iende sambamba na kasi iliyopo ya kuongezeka kwa miradi ya Utalii pamoja na ile ya Sekta nyengine inayowekezwa katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechapuzwa kuendelea kuongeza nguvu zaidi katika uimarishaji wa Miundombinu ili iende sambamba na kasi iliyopo ya kuongezeka kwa miradi ya Utalii pamoja na ile ya Sekta nyengine inayowekezwa katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Zanzibar.
Chapuzo
hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa
inayojishughulisha na ujenzi wa Miradi Mikubwa ya Kiuchumi ya MCC
Overseas LTD ya China Bwana Leo Zou wakati akizungumza na Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye Hoteli ya Sheraton Mjini
Beijing.
Bwana
Leo Zou ambae Kampuni yake ndio iliyotiliana Saini Mkataba na Kampuni
ya Penny Royal kwa ajili ya Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Hoteli ya
Kimataifa ya Daraja la Tano {Five Star } Amber Resort Zanzibar katika
Kijiji cha Matemwe alisema Zanzibar hivi sasa inaeleweka vyema katika
ramani ya Dunia.
Mwenyekiti
huyo wa Kampuni ya MCC Overseas alimueleza Balozi Seif na Ujumbe wake
uliopo Nchini China kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku Tano kwamba
Zanzibar lazima iwe makini katika kuandaa mipango imara ya miundombinu
itakayokidhi mahitaji halisi ya ongezeko kubwa la wageni.
Bwana
Leo Zou alisema siku chache alizokuwepo Visiwani Zanzibar ameshuhudia
ongezeko kubwa la idadi ya wageni wanaoingia kwa ajili ya shughuli za
Utalii pamoja na Uwekezaji tokea kufunguliwa njia za Uwekezaji katika
miradi mingi ya sekta ya Utalii.
Mwenyekiti
huyo wa Kampuni ya MCC - Overseas alimuhakikishia Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar kwamba Uongozi wa Taasisi hiyo umeridhika na mazingira
mazuri yaliyopo Zanzibar yanayotoa fursa za uwekezaji kwa Taasisi na
Makapuni ya Kigeni kushawishika kutaka kuwekeza miradi hyao.
Alisema
MCC Overseas mbali ya kujenga mradi wa Hoteli wa Amber Resort Zanzibar
lakini pia iko tayari kuwekeza miradi yake mengine katika sekta ya Umeme
na huduma za Maji safi na salama.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Miradi ya Mafuta na Gesi Asilia pamoja na kukamilika kwa ujenzi
wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar ni miongoni mwa juhudi
zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uimarishajhi
wa miundombinu.
Balozi
Seif hatua hiyo itahamasisha wawekezaji katika sekta ya usafiri wa Anga
kuongeza safari zao za moja kwa moja hadi Zanzibar kutoka nchi ya Falme
za Kiarabu { UAE } na zile wa Bara la Asia ili kuongeza kasi ya Utalii.
Aliueleza Ujumbe wa Viongozi hao wa MCC Overseas kwamba watalii na wageni wanaoingia kwa wingi Zanzibar wakati huu ni wale wanaotoka katika Mataifa ya Ulaya hasa Nchi ya Italy.
Alielezea
faraja yake kutokana na Shirika la Ndege la Uturuki hivi karibuni
kusaini mkataba wa Ndege zake kuanzisha safari za moja kwa moja kutokea
Nchini Uturuki hadi Zanzibar.
“
Tumeshuhudia hivi karibuni utiaji saini Mkataba uliofungwa na Uongozi
wa Shirika la Ndege la Uturuki kuanzisha safari za ndege zake moja kwa
moja hadi Zanzibar kitendo kinachotuonyesha mabadiliko ya watalaii
watakaoingia Zanzibar badala ya wale pekee tuliyowazoea kutoka Italy ”.
Alisema Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Kampuni hiyo ya MCC -
Overseas kwa hatua yake ya awali ya kuanza kwa matengenezo ya Ujenzi wa
mradi wa Hoteli ya Amber Resort uliyopo Matemwe.
Balozi
Seif alifahamisha kuwa mbali ya kuongeza Mapato ya Taifa lakini pia
kuanza kwa harakati hizo kutatoa fursa za ajira kwa Vijana wazalendo
zinakazowasaidia kupunguza ukali wa maisha.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments
Post a Comment