Diwani wa Bungu, Mhe. Ramadhan Mpendu (kushoto) akihamasisha
wakazi wa Bungu kujiunga na VSOMO inayowezesha kutoa mafunzo ya ufunzi stadi
kutoka VETA kwa njia ya simu za mikononi kwa kushirikiana na Airtel katika
semina iliyofanyika katika ofisi ya kata ya Bungu katika wilaya ya
Rufiji.
**********************************************************
Mamlaka ya
ufundi stadi Nchini VETA kupitia chuo chake cha VETA Kipawa kimeanza kutoa
mafunzo ya ufundi wa Umeme, ufundi wa simu za Mkononi, ufundi wa kuchomelea
vyuma (welding) n.k katika vijiji
vitakavyo nufaika na mradi wa Umeme Vijijini (REA) kwa kutumia njia ya mafunzo
kwa njia ya simu ya Mkononi (VSOMO), mfumo uliobuniwa kwa pamoja kati ya Airtel
na VETA na kuzinduliwa June 7, 2016.
Hayo yamesemwa
katika uzinduzi wa program ya VSOMO uliobeba kauli mbiu (FURSA INAKUFUATA
ULIPO) uliofanyika viwanja vya ofisi ya kijijini za kata ya Bungu Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani
na Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa Eng.
Lucius Luteganya kwamba “mfumo huu wa mafunzo (VSOMO), wanafunzi watajifunza
nadharia kwa njia ya simu ya mkononi (smartphone) kwa kupakua bure mfumo huu wa
VSOMO kutoka kwenye google play store ambapo msomaji atafanya mitihani ya kupima
ufahamu wa somo kwa kutumia simu hiyo ya mkononi na hatimae mafunzo kwa vitendo
kwa walio faulu nadharia, mafundi wa chuo cha VETA watawafuata wakiwa na
karakana inayotembea (Mobile workshop) ili kutoa mafunzo ya vitendo kwa wale
waliofaulu nadharia tu.
Eng, Luteganya
aliongeza kuwa “Katika makubaliano yaliyofikiwa na wadau wengine, EWURA watatoa
leseni kwa mafundi wa umeme watakaohitimu katika kozi ya UMEME, SIDO watatoa
mafunzo ya ujasiliamali yanayoambatana na fursa za umeme kwa wanavijiji husika,
na mwisho orodha ya wahitimu itapelekwa REA, TANESCO na kwenye Board ya wakandarasi
ili mashirika na makampuni yatakayopewa kandarasi yaweze kuwatumia katika
kujenga miundo mbinu (Wakandarasi), kutunza miundo mbinu (Tanesco) na REA”.
Katika
uzinduzi wa Program hii (FURSA INAKUFUATA ULIPO) kwa wakazi wa vijiji vya Kata
ya Bungu wilaya Rufiji Mkoani Pwani wadau wote VETA wakiwakilishwa na Mkuu wa
Chuo cha VETA Kipawa Eng. Lucius Luteganya na timu yake, Airtel wakiwakilishwa na Bi. Hawa Bayumi Manager wa
Airtel Fursa, SIDO wakiwakilishwa na Mr. Stephen Bondo, EWURA wakiwakilishwa na Chief Inspector Eng.
Simon , Tanesco wakiwakilishwa na Eng. Mbwiga Chimala walipata mapokezi makubwa
kutoka kwa wananchi na viongozi wa kata ya Bungu.
Nao baadhi ya Wananchi wameeleza kufurahishwa na mpango huo
na kwamba mara nyingi wamekuwa wakishindwa kupata mafunzo kutokana na vyuo vya
ufundi kuwa mbali lakini kwa sasa wanaona fursa hii imewafuata hivyo ni jambo
muhimu katika maisha yao."Kusema ukweli haya mambo kwetu ni muhimu sana na
mara nyingi tumekuwa tukishindwa kupata mafunzo kama haya kutokana na
upatikanaji wake kuwa mgumu maana vyuo hadi usafiri kwenda Dar es salaam jambo
ambalo ni gumu kwetu," Khamis Shaban-Mkazi wa Bungu
Nae Ramadhani Mpendu Diwani wa Kata ya Bungu ameeleza
kufurahishwa na mpango huo huku akiwasisitiza viongozi wenzake kutoa elimu kwa
wananchi ili wachangamkie fursa.hiyo muhimu na kuondoa malalamiko ya kuporwa
ajira. Mfumo huu wa mafunzo utaendelea katika vijiji vingine vitakavyonufaika
na mradi huu.
No comments
Post a Comment