Mahakama ya mkoa wa Dodoma imewahukumu watu wawili kifungo cha
miaka ishirini gerezani kila mmoja kufatia kutiwa na hatiani kwa kosa la
kukutwa na meno ya tembo eneo la Atta wilaya ya Kondoa mwaka 19/ 5/
2014.
Waliohukumiwa kifungo hicho ni pamoja na Khamis Juma na Hussen Juma wakazi wa wilaya Kondoa.
Wakili wa serikali Consntatin Kikula wakishirikiana na wakili wa kutoka hifadhiu ya taifa ya tarangile Linus Bugabe waliiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na wahifadhi wa mbuga ya tarangire kwa kushirikiana na polisi wilaya ya bababti
Ambapo walikutwa na meno mawili ya tembo yakiwa uzito wa kilo 43 yenye thamani ya shilingi milioni 38 laki tano elfu 49 na mia tano hivyo kuiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa hao ili liwe fundisho kwa wengine.
Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi mfawidhi Mh. Fovo alikubaliana na maelezo ya upande wa serikali kwa madai kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiendelea kushamili hivyo kulisababbishia hasara taifa.
Sambamba na kumalizika kwa wanyama hao hivyo kutupilia mbali hoja ya upande wa utetezi wa washitakiwa hao waliokuwa wakitetewa na wakili msomi Godfrey Wasonga.
Chanzo Startv

No comments
Post a Comment