Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema, wao kama wachezaji walijitahidi sana kwenye mchezo wa jana dhidi ya Malawi wakiwa ugenini licha ya kufungwa goli moja wakaiwa ugenini Cannavaro ameongeza kuwa walicheza kwa nidhamu ya juu kuhakikisha hawapotezi nafasi ya kuonga mbele.
Cannavaro amesema mpira unakimbia
sana kwenye uwanja wenye nyasi za bandia hivyo iliwalazimu kutumia
nguvu ningi sana kumiliki mpira ukilinganisha na kwenye viwanja vingine.
“Tulicheza kwa nidhamu kwasababu tulikuwa tunahitaji kulinda matokeo ambayo tuliyapata nyumbani”, amesema Cannavaro.
“Uwanja ulitu-cost kwasababu
kwenye uwanja wa nyasi za bandia mpira unakuwa unakimbia sana, watu wa
nje hawawezi kujua hilo, inamaana hata ukitaka kumiliki mpira inabidi
utumie nguvu na uupoze sana mpira lakini tumejitahidi”.
Cannavaro amesema watu wachukulie
mchezo kati ya Stars dhidi ya Algeria ni wa kawaida lakini akisisitiza
Stars lazima itumie faida ya kuanzia nyumbani ili ipate magoli ya
yatakayowasaidia kwenye mechi ya marudiano.
“Watanzania inabidi watuombee dua
kuelekea mchezo wetu dhidi ya Algeria, tuchukulie ni mchezo wa kawaida
na kwasababu tunaanzia nyumbani inabidi tupate magoli mengi ili tuweze
kufuzu kwenye hatua ya makundi”.
No comments
Post a Comment