YANGA
kwa sasa hawashikiki katika michuano ya Ligi Kuu ya Soka ya Vodacom
Tanzania Bara (VPL), kutokana na kuwa na washambuliaji moto na ukuta wa
chuma hali ambayo imeanza kuwatia hofu wapinzani kwa kila timu kwenye
ligi hiyo.
Katika
mechi tano ambazo wamecheza, Yanga wameshinda zote huku safu yake ya
ushambuliaji ikionekana kuwa moto wa kuotea mbali baada ya kupachika
mabao 13, ikiwa ni wastani wa ushindi wa mabao 2.6 katika kila mechi.
Wakati
safu ya ushambuliaji ikionyesha makali hayo, safu ya ulinzi ya klabu
hiyo ya Jangwani inaonekana kuwa kama ukuta wa chuma kwani hadi sasa
ndiyo timu pekee ambayo imefungwa bao moja tu kwenye msimamo wa ligi
hiyo.
Licha
ya kwamba wanafungana kwa pointi na mabingwa wa Afrika Mashariki na
Kati, Azam FC, wote wakiwa na pointi 15, Azam wao wamefunga mabao tisa
(9) na kufungwa mawili hiyo wanakuwa na wastani wa mabao saba (7),
wakati Yanga wao wanakuwa na wastani wa mabao 12.
Yanga
ambayo juzi ilivunja mwiko kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kwa
kuivurumisha Mtibwa Sugar mabao 2-0, ilifungwa bao pekee kwenye ligi
hiyo katika mechi dhidi ya KJT Ruvu ambapo mabingwa hao watetezi
waliibuka na ushindi wa mabao 4-1.
Chanzo:Bingwa
No comments
Post a Comment