Njombe
habari na John Banda
WATANZANIA wametakiwa kuwapelewa watoto wao katika vyuo
mbalimbali vya ufundi stadi elimu inayo zalisha ajira nyingi kuliko vyuo
vikuu hapa nchini ili kuepukana na tatizo la ajira.
Inadaiwa kuwa watu wanaojiajiri ni wengi wanao toka katika
vyuo vya ufundi kuliko wanano maliza vyuo vikuu kutokana na wanao toka
vyuo vikuu wanategenea kuajiliwa huku wa vyuo vya ufundi wakijikita
kujitengenezea ajira na kuachana na utegemezi kutoka kwa wazazi.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa bodi ya vyuo vya Veta
nyanda za juu inayo jumuisha mikoa ya Iringa, Ruvuma na Njombe, Kabaka
Ndenda, katika mahafari ya kwanza kwenye chuo pekee ya wilaya cha Veta
Makete, alisema kuwa vijana wengi wanao maliza katika vyuo vya ufundi
wanauhakika wa kujiajiri kuliko wanao enda vyuo vikuu.
Amesema kuwa wananchi wamekuwa wakiona ni bora kumpeleka mtoto wake katika chuo kikuu kuliko kumpeleka katika vyuo vya ufundi.
Mkuu wa chuo hicho Ramadhani Sebo amesema wanafunzi hao
wanaenda kuajirika licha ya kuwa na changamoto za vifaa vya kufundishia
katika baadhi ya fani zinazo fundishwa katika chuo hicho.
Ameongeza chuo hicho kilianza na kozi mbili na sasa kina kozi 4 huku kikifundisha masomo mtamboka.
Wanafunzi nao hawakua mbali kuiomba serikali kuongeza uwezeshwaji kwa vijana wanaojiajiri
No comments
Post a Comment