Licha
ya uhasimu wao mkubwa enzi zake akiwa kocha wa Manchester United, Sir
Alex Ferguson amempongeza Arsene Wenger kwa kuendelea kubaki kuwa meneja
wa Arsenal kwa kipindi kirefu.
Wenger
ambaye siku za hivi karibuni, amekuwa katikacpresha kubwa kutoka kwa
mashabiki kutokana na kutofanya usajili wa uhakika na vile vile kukosa
kombe la EPL tangu mwaka 2004.
Lakini
Ferguson anaona dhahiri shahiri kuwa kutakuwa na tatizo kubwa pale
Arsene Wenger atakapoondoka klabuni hapo, kama ilivyotokea kwa
Manchester United.
Arsene Wenger
Sir Alex Ferguson (kulia) na Arsene Wenger.
Aliiambia ESPN
kuwa: 'Ni kama ilivyotokea kwangu endapo nisingeweza kuisogeza mbele
klabu baada ya timu ya mwaka '94 ama '99, pengine ningepata tatizo kama
alilonalo Arsene, lakini hata hivyo bado ameendelea kushikilia misimamo
yake, amebaki na kile anachokiamini.
'Wkati
wote ambao presha hii inatokea - huwa nawaambia marafiki zanguu
wachache kwamba- hivi watampata nani ambaye ataweza kumrithi Arsene
Wenger, uanjua, ni nani watampata ambaye atakuwa bora zaidi ya Arsene
Wenger?
'Na ndiyo maana hawamfukuzi, ndiyo maana wameendeka kubaki naye.'
No comments
Post a Comment