Thomas Ulimwengu (kulia) akimkimbilia Mbwana Samata kushangilia goli la pili baada ya kuifungia Stars wakati ikicheza dhidi ya Malawi
Timu
ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ chini ya kocha mzalendo Charles
Boniface Mkwasa leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya
Malawi kwenye mchezo wa awali uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa kusaka
tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Mbwana
Samata alianza kuiandikia Stars goli la kwanza dakika ya 19 kipindi cha
kwanza akiunganisha pasi ya mchezaji mwenzake wa TP Mazembe Thomas
Ulimwengu.
Stars
baada ya kupata goli hilo waliamka na kuanza kucheza mpira na kutawala
mchezo kwa asilimia nyingi katika kipindi cha kwanza na kutengeneza
nafasi kadhaa za kufunga lakini nafasi hizo hazikutumiwa ipasavyo kwani
bado walipoteza nafasi nyingi za kufunga.
Thomas
Ulimwengu aliiandikia Stars bao la pili dakika ya 22 kipindi cha kwanza
akimalizia mpira uliomshinda kipa wa Malawi uliopigwa na Haji Mwinyi na
kuihakikishia timu hiyo kupata ushindi wa kwanza tangu imeanza kunolewa
na Mkwasa aliyepokea kijiti hicho toka kwa kocha Mart Nooij
aliyetimuliwa mwezi Julai mwaka huu.
Kabla
ya mchezo wa leo, Stars ikiwa chini ya kocha Mkwasa imetoka sare kwenye
mechi mbili za mashindano na kupoteza mchezo mmoja wa kirafiki.
Mrisho
Ngassa (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa Malawi wakati wa mchezo
kati ya Stars dhidi ya Malawi kuwania kukata tiketi ya kucheza fainali
za kombe la dunia mwaka 2018
Sare
ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Uganda mchezo uliochezwa Uganda kuwania
kufuzu kucheza fainali za Afrika kwa wacheaji wa ligi za ndani (CHAN)
huku wakitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu
fainali za mataifa ya Afrika.
Stars
ikiwa chini ya Mkwasa ilipoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Libya kwa
goli 2-1 wakati ikiwa Uturuki kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.
No comments
Post a Comment